Idrissou02
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 354
- 656
Usimtumie hela in cash..Nipo na ajira nashkuru mungu inayofanya nisogeze maisha. Nina mshahara mdogo tu lkn kwa ubachela wangu unanitosha.
Mdingi wangu (mzazi pekee nliyebaki nae kwa sasa) ana kipato cha uhakika na hana shida ya pesa ndogondogo. Kipato chake ni mara 5 zaidi ya changu kwa mwezi.
Nimekuwa nikiumiza sana kichwa kwamba inanipasa kumtumia mzee percent ya kipato changu kwasababu tu ni mzazi ama nikaushe niweke akiba inisukume kwenye harakati zangu
Mimi ni mzazi.Watoto, Mke wako na wewe kama wote wako sawa Wazazi labda ndiyo wafwatie, lkn wazazi wasiwe kipaumbele chako na wala usiwaendekeze watakupoteza, wao walishakuwa na maisha yao na wewe kuwa na yako, angalia Mke na watoto kama mmejaliwa kwanza!
Mimi kwa upande wangu wote ni vipaumbele vyanguWatoto, Mke wako na wewe kama wote wako sawa Wazazi labda ndiyo wafwatie, lkn wazazi wasiwe kipaumbele chako na wala usiwaendekeze watakupoteza, wao walishakuwa na maisha yao na wewe kuwa na yako, angalia Mke na watoto kama mmejaliwa kwanza!
Mimi ni mzazi.
Nafahamu raha ya uhusiano na mawasiliano bora kati ya mzazi na mwanae.
Mwelewe/msome zaidi mzazi wako.
Wazazi tunatofautiana.
Kuna wanaopenda kupewa pesa, kuna wanaopenda zawadi, kuna wanaopenda pesa na vitu.
Kuna tunaopenda MAWASILIANO THABITI NA MAENDELEO ya wanetu.
Namaanisha tunatamani kuthaminiwa.
Naunga mkono kujijenga na kujenga familia yako kwanza kwa kuzingatia uwezo wa mzazi.
Mbona mada ni nzuri na watu wamechangia vizuri kabisa?JF ya zamani itarudi lini ndugu Mero? Jukwaa hili lilikuwa muhimu na mada nyingi zilikuwa za kujenga na si kupotosha kama hii!