Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Budget ni muhimu inafavour!!.. mfano wangu huwa nafanya hivi

Kipato kwa ujumla = 100%

Kodi za Pango biashara & makazi = 10%
Chakula = 25%
Mavazi = 5%
Usafiri = 8%
Ada za madogo = 10%
Akiba = 30%
Viburudisho = 2%
Bima afya nk = 7%
Mengineo = 3%
 
Kwa upande wangu naona ni ngumu sana kwa mtanzania au mwafrika kuishi kwa bajeti
Sabu maisha yetu hayana mpangirio sasa inakua ni ngumu sana kuishi kwa bajeti

Umepanga kwa sku utatumia usafiri shiling elf2 ila unafika kituoni daladala wamegoma inabidi upande boda bajeti imekufa
Umepanga utatumia kwa mwezi mzma lk 1 ila unapigiwa simu nyumban kuna msiba, au kuna mtoto wa dada hana karo inabidi uchangie
Umepanga chakula elf10 mwezi mzma inafika katikati ya mwezi mahindi yamepanda bei mchele umepanda bei sukar imepanda bajeti imebadilika

Kuishi kwa bajeti ni kuzuri ila ni mara chache sana unaweza kuishi kulingana na bajeti yako sababu ya mfumo wa maisha yetu
 
Familia ina ukubwa gani?
 
Hayo unayotaja unayaweka ktk bajeti ya dharura.
 
Kwa wenzetu maisha yao sometimes yanaongozwa na mikopo unasikia credit card maana yake mtu anaweza pata huduma akalipa baadae
Ila kwa afrika na Tanzania maisha yetu kila kitu kinategemea cash pesa taslimu.

Lakin pia kwa wenzetu serikal zao zinajua kusimamia masula la upandaji wa bei wa bidhaa ni ngumu sana kwa wenzetu bei za bidhaa kupanda hovyo hovyo ila kwa uku kwetu bei zinabadirika mara kwa mara na bila utaratibu wwte.

Kuishi kwa bajeti ni vitu vingi sana huchangia ila mtu uweze kuishi kwa bajeti na kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako izo unaweza kuzikabiri ila kuna sababu zilizo nje ya uwezo wako izo ni ngumu kuzikabiri.
 
Kweli watu hatufanani, mimi kuishi bila bajeti siwezi. Kila kitu kinakwenda kwa hesabu hapa tu nipo kwenye mipango ya June huko.

Sikiliza, anza kwa kununua vitu kwa jumla hasa vyakula (Mchele, Mafuta, Maharage, Sukari n.k)
Kisha vinginevyo kama nyanya, vitunguu n.k nenda Ilala fungasha jaza friji na ukiona vyema nunua kuku na samaki weka kwenye friza utakuja kuniambia.

Hapa kinachonipa stress ni skin care yangu inaisha na bajeti yake imechangamka kidogo, basi.
Wife material
 
Jaribu Taimur product search huko Instagram utaipata.. mimi mwaka wa 3 huu naitumia niko very soft na rangi yangu haichubui .. ukiwatafuta watakushauri kwanza baada ya kuona ngozi yako but mimi haijanikataa
Shukrani
 
Ma bro hamjambo.......

Hili jambo huwa linanitafakarisha sana, najaribu jaribu bajeti siku chache mara napoteana, ila kiukweli siku nnazoishi kwa bajeti naona kabisa matumizi ya pesa yanakuwa vizuri.

Bajeti namaanisha kuanzia eneo la chakula nyumbani, yani unapanga matumizi na kuishi ndani ha matumizi.

Baada ya hapo matumizi binafsi mwezi huu labda bajeti ya wanja, lipstic pochi ni kiasi flani na uishi humo. Hivi hii kitu inawezekana??? Kuna watu wanaishi na bajeti hivi labda hata mwezi???

Kama inawezekana nipo serious kabisa naomba mtu anifundishe hatua kwa hatua, ikibidi mtu aniandikie, kati ya vitu nnavyotamani sana kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu ni kuishi kwa bajeti ila sijafanikiwa 😢

Natanguliza shukrani.
Watu wasio zingatia bajeti ni wale wenye kipato kikubwa sana kiasi kwamba hata atumie kiasi gani ukwasi wake uko pale pale
Au watu wanaishi chini ya watu wengine

Lakini kama unakipato unga unga basi unaishi kwa bajeti vinginevyo kipato chako kingekua kinapelea kila mwezi

Inawezekana wewe una maanisha kufanya savings
 
Hivo hivo kuishi kwa bajeti, kupanga mahesabu na kufanya matumizi kwa mpangilio
 
Ilu uishi Kwa bajeti lazima Kwanza uwe na bajeti mkuu yenye maLengo, afu izo bajeti ndogo ndogo ndo zitafata hapo.
 
Back
Top Bottom