Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Bila bajeti sitoboi.
1. Vyakula vya mwezi unga, Mchele, mafuta ya Kula, sukari, maharage.
2. King'amuzi, umeme, ela ya taka, ulinzi shirikishi na maji ( kwa mwezi).
3. Mahitaji ya watoto kama nauli za shule, pampas na maziwa (monthly).
4. Vitui kama mkaa na gesi ni kwa miezi mitatu mara moja.
5. Matumizi yangu yangu ya lazima kama vile nauli na Kula nikiwa job. (Monthly)
6. Pesa ya kuacha home week days kwa ajili ya matumizi ya home km mboga na vitafunwa au matunda. (Monthly)
7. Mishahara hususani dada wa kazi (monthly)
8. Matumizi mengineyo home ya mama mtu na watoto kama vile kusuka n.k
9. Dharura.

Huo ndio mwongozo wangu wa mwezi. Hiyo bajeti inakula karibu asilimia 90 ya ninachokipata kwa mwezi.
Bora nimezaliwa wa kike… kwakweli na huu ubahili nisingeweza kutoa hela zote hizo weeeee poleni sana wanaume… mtakula kwa jasho mpk mufe
 
Okay walau chakula inapangika....

Haya matumizi mengine, cosmetics nguo, saloon etc hii je? Unaipigiaje hesabu?
Salon inategemea unasukaje wenginee ni kila baada ya mwezi kama ni nywele za hela au za mkono kwa wiki unasuka mara 2 uzuri

siku hiz kuna style nzuri za natural hair
Swala la vipodozi sizani kama kila mwezi unanunua
Kwa mimi ambae sio mtu wa kujipamba sana nina skin care yangu nanunua kila baada ya miezi 5.. nguo sinaga bajet ikitokea nimependa basi nanunua sinaga siku maalumu ya kununua nguo
 
Mi sisuki sipendi kusuka, huwa nanyoa
 
Hii ndio hatua ya kwanza unayopaswa kufanya kabla ya kupanga bajeti. Andika Kila kitu unachonunua. Uzuri siku hizi Kuna apps zinazorahisisha Hilo. Baada ya mwezi au miwili tumia data hizo kupanga bajeti. Kumbuka bajeti ni Sheria, utofauti ni kwamba haijapangwa na bunge ni Sheria uliyojipangia mwenyewe. Itii. Bila budget sio rahisi kutoboa.
Kabisa mkuu, kuandika kutarahisisha ujue hasa madhaifu yako
 
Samahani naomba nicheki now pm tuongee jambo..
Hayo ndio mambo yangu mpaka nafikia sasa nakua millionea ni kwa sababu ya bajeti..
Kama upo seriously nichek nikufundishe kanuni moja inaitwa PERSONAL TRAINER KIT
Tufundishe na wengine hapa ndugu.
 
Kama muuzaji ana lipa namba,natumia hiyo,ila kama hana nikitoa pesa basi nitaweka note ili iwe rahisi,japokuwa kiukweli tokea nianze kuishi peke yangu almost miaka 4 sasa,sijawahi kununua nyanya
Unakula mboga zisizo na nyanya?
 
Back
Top Bottom