Japo ni kipengele kuishi kwenye bajeti ila kuanza anza kua unaandika matumizi yako kila siku kuanzi siku unapata kibunda.
Andika unatoa kiasi gani, umenunua nini na nini. Kama ni mtu ambae fuba linaisha hata tarehe 10 haijafika basi pitia daftari lako jiasses ni wapi umezingua, kitu gani umenunua na hakikua na umuhimu? Usijionee aibu na kujipa excuses za uongo jichane hapa ulizingua.
Utaona tu pesa yako inakimbilia wapi zaidi, kwangu niligundua kula msosi mgahwani kunamaliza mno pesa kindezi, nikaanza kunua vitu kwa jumla na kutia ndani na kupika mwenyewe sometimes kupitia darasa huru la
Mwachiluwi .
Vile vyote ambavyo umeona vinakula sana pesa, viandalie njia mbadala ya kupunguza matumizi yake. Ni mpenzi sana wa bolt/boda hata mahali pasipo na ulazima wa boda, punguza. Ni mlaji hovyo wa pweza, ukwaju, juice,soda au bia bila mpangilio kila ukijiskia, punguza/control hiyo hali.
Notebook yako itafanya ujue mengi kuhusu wewe, ujue ni mianya ipi ambayo hukuizingatia ila inakula pesa kimyakimya baada ya hapo budget utaipanga kulingana na vipaumbele vyako.