Huwa najaribu naishia njiani. Kitu kimoja ambacho huwa sitetereki ni kuhakikisha ndani ya nyumba kuna chakula na mahitaji muhimu ya kutosha. Nanunua in bulk vitu kama vyakula (mchele, unga, maharage, samaki, nyama, kuku, mafuta ya kupikia) gas, mkaa, na makorokoro mengine ninayoweza kuhifadhi kwenye fridge. Nahakikisha umeme, maji, DSTv haikati. Vitu vingine vidogo vidogo kama vitafunwa, maji ya kunywa, mboga za majani budget yake haikosekani. Huwa naomba Mungu tu kusitokee emergency itakayonifanya kutumia pesa nyingi. Sijawahi kuwa na budget ya nguo, cosmetics wala nywele!!! Hivyo havinipi shida. Sijanunua nguo mwaka wa 6 huu!!! Sipaki cosmetic yoyote na nywele napata olive oil tu.