mie pia ni mhanga wa hili, kwa mfano nampa wife laki 4 ya mwezi mzima,
kiasi kilichobaki huwezi amini wiki moja au mbili sina kitu 😁, naanza kujibebisha kwa wife mf. " mama ( ) embu niazime elf 5000 nataka nikatoe ndevu kidogo" ataanza kulalama kwamba "we hurudishi mme wangu nakujua" atapiga tantalilia mwishowe ananipa na sirudishi kweli 🤣,, mvurugaj mkubwa wa bajet ni mimi, wife yuko makini sana,,,
kuna mwezi akasusa kabisa😁, akasema huu mwezi tunataka pesa ya bajet nzima ukae nayo wewe (mimi) nikasema poa ,, walinikomoa huo mwezi ,, nimetulia job inaingia sms " tuwaishie mboga " naichek ile sms naijibu poa,, naendelea storika kwanza , nampigia boda "nani embu pita buchani wapeleke kg 1 "
ukifika home unaambiwa mme wangu nyama aliyoleta boda kapigwa ina mifupa kishenz,, 🤔🤔,,, naambiwa bora ungeenda mwenyewe,,
HIZI BAJET ZANITESA KISHENZI,, naweka kambi niambulie kitu,, ila nishajijua mie ni tatizo,, kuna siku nawaza au nimpatie Mshahara wote 😆,, si kuitwa mume bwege 😳 huku,,