Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Okay walau chakula inapangika....

Haya matumizi mengine, cosmetics nguo, saloon etc hii je? Unaipigiaje hesabu?

Nguo uwe na bajeti ya mwaka kwa familia yako. Mimi huwa nina bajeti ya kwangu ni 1m kwa mwaka kwa nguo na viatu; Hapo ni kubwa sababu ya suti, kazi zangu zinahusisha uvaaji wa suti sana. Na kila mtoto namuwekea laki 2 bajeti ya mwaka kwa nguo na viatu na tunaenda wote nawanunulia kila mtu chake. Hizi ni kwa nguo na viatu vya nyumbani tu hazihusishi za shule wala sikukuu.
 
bajeti ndio matumizi yenyewe,sijaelewa unavyosema kuishi bila bajeti unamana gani?

ondoa shaka binti yangu mi naona uko vizuri mradi unafanya matumizi basi sioni shida iko wapi
Kuishi kwa bajeti maana yake nataka kujua na kuishi mwezi huu nitatumia mchele elf 10, unga elf 10 saloon 10, viatu 10 maana yake mwezi ukiisha hivyo vitu vyangu vitembee humo na sio kutumia tumia badala ya hiyo 40 ifike 95 umenielewa???
 
Muda wako wa kuamka ni mzuri sana.
Jitahidi sana kitu cha kwanza unapoamka asubuhi ni kumuomba Mungu wako kwa imani yako.
Fanya hivyo minimum siku 40.....then rudi hapa tupe mrejesho
Ahsante kwa kunikumbusha, kuna nguvu kubwa katika kuomba Mungu vitu v...huwa nina muda wa kufunga na kuomba ila huwa sifanyi kila siku, ahsante.
 
Ma bro hamjambo.......

Hili jambo huwa linanitafakarisha sana, najaribu jaribu bajeti siku chache mara napoteana, ila kiukweli siku nnazoishi kwa bajeti naona kabisa matumizi ya pesa yanakuwa vizuri.

Bajeti namaanisha kuanzia eneo la chakula nyumbani, yani unapanga matumizi na kuishi ndani ha matumizi.

Baada ya hapo matumizi binafsi mwezi huu labda bajeti ya wanja, lipstic pochi ni kiasi flani na uishi humo. Hivi hii kitu inawezekana??? Kuna watu wanaishi na bajeti hivi labda hata mwezi???

Kama inawezekana nipo serious kabisa naomba mtu anifundishe hatua kwa hatua, ikibidi mtu aniandikie, kati ya vitu nnavyotamani sana kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu ni kuishi kwa bajeti ila sijafanikiwa 😢

Natanguliza shukrani.
Inawwzekana kabisa, cha msingi andaa zero - based budget, hakikisha kipato chako unachotarajia kupata huachi hata senti tano ambayo haijapangiwa matumizi, muda unapopokea hiyo hela unakuwa huna tena hela theoretically, ishi humo, chochote za ziada kitakachojitokeza, jitahidi kutumia njia nyingine kutatua, kama vile kukopa, kutumia mfuko wa dharura au kutumia hela zinazotokana nje ya mfumo wako rasmi wa kipato kama vile rushwa (kwa wale wala rushwa), kuhongwa, zawadi, n.k

Budget yako isiache haya
1. Saving & investment
  • Mfuko wa dharura
  • malengo
  • uwekezaji

Kuishi kwa budget kunakuhakikishia uhakika wa kuishi kwa kile ulichonacho, kinachotakiwa ni nidhamu ya kufuata uliyojipangia
 
You are right Ila malalamiko kama vile ni fist person.

Sijali sana, nilitaka tu kuchana.

Wakati mimi naishi na mwanamke last time in my 20’s alikuwa hajui gharama za nyumbani na alikuwa anafanya kazi.

Sasa baba yake akiwa na shida alikuwa anantumia hela mpaka marehemu baba yake akawa anaogopa. Isije kuwa anamfanya binti yake kufanya mambo ya ajabu ili amtumie hela.

Kumbe wala mimi nilikuwa sigusi hata shillingi yake atajuwa atakavyotumia hela yake. Na kwake haikuwa na kazi zaidi ya kumtumia baba yake na kuwanunulia wadogo zake viwalo.

Same, mama yangu alikuwa na shughuli zake; lakini changamoto za ada zilikuwa zake ambazo sidhani kama maza alikuwa anazijua.

It saddens me kuona mwanamke analalamika maisha, nabaki najiuliza who did she marry kwa malezi yangu.

Anyway mta ji JJ ngonja nikatafute ugomvi kwenye siasa.

Binafsi siwezi kuwa na mwanamke mwenye kuhaha shida, I won’t allow that

mbona kama unajisifia sana kiongozi! Angalia sana aliyekupa wewe ndiye anayeweza kukushusha pia; unaweza kuamka kesho asb uko hohe hahe...

Tumuogope Mwenyezi Mungu na tuwe wanyenyekevu tusidharau wenye vipato vidogo.. kama umezaa watoto wa kike au unaye dada basi jiandae kwa haya unayowasimangia wenzako humu. Karma huwa haikosei njia..
 
mbona kama unajisifia sana kiongozi! Angalia sana aliyekupa wewe ndiye anayeweza kukushusha pia; unaweza kuamka kesho asb uko hohe hahe...

Tumuogope Mwenyezi Mungu na tuwe wanyenyekevu tusidharau wenye vipato vidogo.. kama umezaa watoto wa kike au unaye dada basi jiandae kwa haya unayowasimangia wenzako humu. Karma huwa haikosei njia..
Hata usimchukulie serious.....😁
 
Back
Top Bottom