Bila bajeti sitoboi.
1. Vyakula vya mwezi unga, Mchele, mafuta ya Kula, sukari, maharage.
2. King'amuzi, umeme, ela ya taka, ulinzi shirikishi na maji ( kwa mwezi).
3. Mahitaji ya watoto kama nauli za shule, pampas na maziwa (monthly).
4. Vitui kama mkaa na gesi ni kwa miezi mitatu mara moja.
5. Matumizi yangu yangu ya lazima kama vile nauli na Kula nikiwa job. (Monthly)
6. Pesa ya kuacha home week days kwa ajili ya matumizi ya home km mboga na vitafunwa au matunda. (Monthly)
7. Mishahara hususani dada wa kazi (monthly)
8. Matumizi mengineyo home ya mama mtu na watoto kama vile kusuka n.k
9. Dharura.
Huo ndio mwongozo wangu wa mwezi. Hiyo bajeti inakula karibu asilimia 90 ya ninachokipata kwa mwezi.