Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Kwanza unatakiwa kuwa na Kipaumbele;

Kama ni Mtumishi hakikisha nauli inakuwa sehemu ya Kipaumbele chako baada ya Chakula n.k

Kwahiyo unaweza kuandaa Bajeti yako Kwa kuangalia Vipaumbele vyako katika Matumizi yako

Unaanza na Chakula,Usafiri, Mawasiliano (Vocha ya kupiga pamoja na Bando la internet),Kodi,Umeme,Kulipia Kisimbuzi/Visimbuzi,Maji, Vikoba n.k

Baada ya kuandaa Bajeti yako, kumbuka kuweka na fedha ya Dharura na Akiba kisha uanze kutumia kama ulivyoandaa bajeti yako

Ni muhimu kununua vyakula in bulk ili kupunguza gharama na wakati mwingine Kulala njaa Kwa kuishiwa fedha katikati ya Mwezi.

Usipoweza pia kutenga bajeti ya Fedha ya Akiba unaweza kujikuta unafika Umri wetu sisi Babu zenu ukiwa apeche alolo

Kwa maana utajikuta zaidi ya asilimia 99 ya kipato chako ulitumia kula/kuishi bila kujiwekeza
 
Bro huko ulikoniona sio mimi 😂😂😂😂

Hebu anza kunitofautishia hapo
Ili nijue pa kuanzia

Ni wewe yule kwenye uzi wa vitabu 😂😂

Needs ni yale mambo muhimu ambayo huwezi kutoboa bila hayo mfano nguo,chakula,gharama za usafiri,kodi na mengine
Wants ni kama gym,skin care,salon na vitu vinavyofanna na hivyo ambavyo ni kama anasa

Ulishawahi kuwa na utaratibu wa kuandika matumizi yako ya mwezi mzima unaofuata na kuyatathmini?
Matumizi yako makubwa huwa yapo kwenye nini hadi unatoka nje ya budget?
 
kumbe we ni wife material kabisa ndo muache kujiita bro mnakuwa mnatuchanganya...🤣
 
Kuhusu budget ya hela nipo vizuri,situmii hela ambayo sikupanga itumike... Evelyn Salt hajaamua

Bahati nzuri sina mtu yoyote nayetakiwa kumpa hela
Mi kwakweli ni mvuruganooo yani sina matumizi ya kueleweka, mara rambirambi nimenunua mboga hela ya mboga sijui imelipa nini mtaji wa biashara mara nimeununua nguo yani bro ni vurugu 😢😢
 
Kwahyo utaki kuwa tajiri? Kama paswedi yako ya utajiri n kuishi kwa bajeti mbona simpo sana punguza matumizi yasiyo ya lazima sana. Sijasema uache bia bro
Mara ya mwisho nmekunywa bia january.....sina mpango wa kunywa hivi karibuni.

Shida kubwa ni kutokua na mipango yani nikiwa na hela ni matumizi ya ovyo ovyo tu kununua vitu ambavyo hata sikupanga
 
Mara ya mwisho nmekunywa bia january.....sina mpango wa kunywa hivi karibuni.

Shida kubwa ni kutokua na mipango yani nikiwa na hela ni matumizi ya ovyo ovyo tu kununua vitu ambavyo hata sikupanga
Ndio umeacha?

Poor financial planning, hiyo tunayo sana watu wengi hasa tukiwa na fedha. Nikushauri cha kufanya kwa ninaemuona anafanya na amefanikiwa kubadilika na kuendana na bajeti.

Yeye huwa anaandika mapato na matumizi yake, hata akiokota mia anaandika, mwsho wa mwezi anafunga hesabu zake na kuangalia wapi panatumia hela zaidi na kama si muhimu anapunguza kama si kuacha. Nataka nijaribu hii mbinu pia nione matokeo yake.
 
Sijaacha nimepumzika kwanza.....

Labda nianze kupunguza sijui napunguzaje labda nisitembee na hela 😁
 
Back
Top Bottom