Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Hivi inawezekana kuishi kwa bajeti ya kila kitu? Chakula, mavazi, matumizi binafsi, nk?

Japo ni kipengele kuishi kwenye bajeti ila kuanza anza kua unaandika matumizi yako kila siku kuanzi siku unapata kibunda.

Andika unatoa kiasi gani, umenunua nini na nini. Kama ni mtu ambae fuba linaisha hata tarehe 10 haijafika basi pitia daftari lako jiasses ni wapi umezingua, kitu gani umenunua na hakikua na umuhimu? Usijionee aibu na kujipa excuses za uongo jichane hapa ulizingua.

Utaona tu pesa yako inakimbilia wapi zaidi, kwangu niligundua kula msosi mgahwani kunamaliza mno pesa kindezi, nikaanza kunua vitu kwa jumla na kutia ndani na kupika mwenyewe sometimes kupitia darasa huru la Mwachiluwi .

Vile vyote ambavyo umeona vinakula sana pesa, viandalie njia mbadala ya kupunguza matumizi yake. Ni mpenzi sana wa bolt/boda hata mahali pasipo na ulazima wa boda, punguza. Ni mlaji hovyo wa pweza, ukwaju, juice,soda au bia bila mpangilio kila ukijiskia, punguza/control hiyo hali.

Notebook yako itafanya ujue mengi kuhusu wewe, ujue ni mianya ipi ambayo hukuizingatia ila inakula pesa kimyakimya baada ya hapo budget utaipanga kulingana na vipaumbele vyako.
 
Ma bro hamjambo.......

Hili jambo huwa linanitafakarisha sana, najaribu jaribu bajeti siku chache mara napoteana, ila kiukweli siku nnazoishi kwa bajeti naona kabisa matumizi ya pesa yanakuwa vizuri.

Bajeti namaanisha kuanzia eneo la chakula nyumbani, yani unapanga matumizi na kuishi ndani ha matumizi.

Baada ya hapo matumizi binafsi mwezi huu labda bajeti ya wanja, lipstic pochi ni kiasi flani na uishi humo. Hivi hii kitu inawezekana??? Kuna watu wanaishi na bajeti hivi labda hata mwezi???

Kama inawezekana nipo serious kabisa naomba mtu anifundishe hatua kwa hatua, ikibidi mtu aniandikie, kati ya vitu nnavyotamani sana kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu ni kuishi kwa bajeti ila sijafanikiwa 😢

Natanguliza shukrani.
Kupanga Budget sio issue sana, issue ni utekelezaji, hapo ndipo nidhamu ya hali ya juu inatakiwa, binafsi nimegawa budget katika makundi haya;
1)Savings
2)Needs
3)Wants
Savings, akiba, hiyo nina kiasi maalumu kabisa, kabla ya matumizi yoyote natenga akiba pembeni, swala la akiba ni pana sana, lakini inaweza kuwa ni kwa ajili ya lengo lolote ulilokusudia.

Needs, Living, haya ni matumizi ya lazima kwa ajili ya kuishi, yani bila hayo maisha hayaendi, bora ukose chochote lakini sio hayo, mfano chakula, matibabu, bundle N.k, mambo kama school fees, kodi yoteyanaweza kuingia hapa hata kama yanalipwa kwa mkupuo.

Wants, hapa ni kujiachia, pesa yote inayobakia ni kwa ajili ya hapa, mfano bata, mavazi, michango ya kijamii n.k

Hivyo ndivyo navyopanga matumizi yangu, naanza na kundi la kwanza, kisha kundi la pili, na mwisho kundi la tatu, kundi la kwanza na la pili huwa nina kiasi maalumu, fixed, kulingana na kipato, wakati kundi ya tatu linategemea na kiasi kinachobakia.
 
Ma bro hamjambo.......

Hili jambo huwa linanitafakarisha sana, najaribu jaribu bajeti siku chache mara napoteana, ila kiukweli siku nnazoishi kwa bajeti naona kabisa matumizi ya pesa yanakuwa vizuri.

Bajeti namaanisha kuanzia eneo la chakula nyumbani, yani unapanga matumizi na kuishi ndani ha matumizi.

Baada ya hapo matumizi binafsi mwezi huu labda bajeti ya wanja, lipstic pochi ni kiasi flani na uishi humo. Hivi hii kitu inawezekana??? Kuna watu wanaishi na bajeti hivi labda hata mwezi???

Kama inawezekana nipo serious kabisa naomba mtu anifundishe hatua kwa hatua, ikibidi mtu aniandikie, kati ya vitu nnavyotamani sana kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu ni kuishi kwa bajeti ila sijafanikiwa 😢

Natanguliza shukrani.
NATAMANI kufahamu unapokea/kuingiza sh ngapi kwa mwezi na mnaishi wangapi hapo getho kwako.
 
Budget depends on your income.

Then consider preference and choice.

Note: Wants are unlimited.

Changua vitu muhimu,alafu anza kupanga kuanzia matumizi ya siku,wiki adi mwezi.

Mfano.Mchele.
kwasiku 1kg=1000,kwa wiki 7kg=7000 na kuendelea ivo ivo na vitu vingine
 
Mi kwakweli ni mvuruganooo yani sina matumizi ya kueleweka, mara rambirambi nimenunua mboga hela ya mboga sijui imelipa nini mtaji wa biashara mara nimeununua nguo yani bro ni vurugu 😢😢
Weka Malengo na kamwe usinunue/usitumie kitu ambacho hakipo kwenye lengo la muda husika labda iwe ni dharura.
Jifunze kutofautisha matamanio na matakwa yako.
Bajeti nakushauri jaribu bajeti ya wiki kwanza, ukiweza weka iwe wiki mbili, ukiweza weka wiki tatu mpaka ifike kipindi uweze kusimamia bajeti ya mwezi mzima.
KUMBUKA: unaweza kama ukiamua NA maamuzi hayatokamilika bila vitendo.
Penda kuandika sehemu bajeti yako ili upate urahisi wa mapitio kama ukivuruga ili utambue ulikosea wapi ili urekebishe.
 
Japo ni kipengele kuishi kwenye bajeti ila kuanza anza kua unaandika matumizi yako kila siku kuanzi siku unapata kibunda.

Andika unatoa kiasi gani, umenunua nini na nini. Kama ni mtu ambae fuba linaisha hata tarehe 10 haijafika basi pitia daftari lako jiasses ni wapi umezingua, kitu gani umenunua na hakikua na umuhimu? Usijionee aibu na kujipa excuses za uongo jichane hapa ulizingua.

Utaona tu pesa yako inakimbilia wapi zaidi, kwangu niligundua kula msosi mgahwani kunamaliza mno pesa kindezi, nikaanza kunua vitu kwa jumla na kutia ndani na kupika mwenyewe sometimes kupitia darasa huru la Mwachiluwi .

Vile vyote ambavyo umeona vinakula sana pesa, viandalie njia mbadala ya kupunguza matumizi yake. Ni mpenzi sana wa bolt/boda hata mahali pasipo na ulazima wa boda, punguza. Ni mlaji hovyo wa pweza, ukwaju, juice,soda au bia bila mpangilio kila ukijiskia, punguza/control hiyo hali.

Notebook yako itafanya ujue mengi kuhusu wewe, ujue ni mianya ipi ambayo hukuizingatia ila inakula pesa kimyakimya baada ya hapo budget utaipanga kulingana na vipaumbele vyako.
Mkuu mkweli chakula cha kununua kwanza kinamaliza pesa pia hushibi unakula ili usife
 
Kweli watu hatufanani, mimi kuishi bila bajeti siwezi. Kila kitu kinakwenda kwa hesabu hapa tu nipo kwenye mipango ya June huko.

Sikiliza, anza kwa kununua vitu kwa jumla hasa vyakula (Mchele, Mafuta, Maharage, Sukari n.k)
Kisha vinginevyo kama nyanya, vitunguu n.k nenda Ilala fungasha jaza friji na ukiona vyema nunua kuku na samaki weka kwenye friza utakuja kuniambia.

Hapa kinachonipa stress ni skin care yangu inaisha na bajeti yake imechangamka kidogo, basi.
Ujuaje kama yuko Dar, anaweza kuwa yuko NY
 
Tafuta mwanaume wa maana hutojua hata bei ya luku.

Ndio shida yenu ilipo hamjui mwanaume wa maana anafanana vipi.

Kuna wanawake wenzenu hawajui gharama za maisha yao hata chembe kwa sababu wanaume zao wanamaliza kila kitu.

Kuja kuuliza hala budget sijui ya nini maana yake huna mwanaume wa maana.

Mimi wakati nina miaka 20 tu mwanamke wangu alikuwa anafanya kazi, akawa anamtumia hela baba yake mpaka anaogopa. Kwa sababu alikuwa hajui mshahara wake aufanyie nini.

Bills za nyumba zote nalipa mimi na shopping ya chakula nafanya mimi.

Sasa ukikuta limama lizima linahaha budget ya familia linauliza budget, hiyo maku umempa mpuuzi gani kwa umri huo uhahe budget ya familia.

Akili za wanawake zinawatosha wenyewe
 
Sio vizuri na sio sifa ulichoandika hapa. Japo ni haki yako. Huna cha maana cha kusema ni vizuri kukaa kimya. Itakufanya uonekane sio mjinga
 
Mimi siishi kwa bajeti ila nime limit to the maximum matumiz yasio ya msingi. Yan na make sure kila nacho spend on ni kitu cha msingi na kinahitaji hasa hakikwepeki (na emphasize more on the needs na nakua makini sana kuepuka the wants).

Ila yote kwa yote, kila week week ni lazima 1kg ya kitimoto rost hii haina mjadala wala kuulizana mara 2 😂😂
 
Sio vizuri na sio sifa ulichoandika hapa. Japo ni haki yako. Huna cha maana cha kusema ni vizuri kukaa kimya. Itakufanya uonekane sio mjinga
Janamke zee linakuja kulalamika ujinga mnataka kuli entertain.

Angekuwa na mwanaume wa maana hayo sio malalamiko ya mwanamke anaejielewa.

Naishia hapa kwa sababu sio mada zinazo ni-interest

Mama yangu mie hakuwa na elimu kama huyu mleta mada anavyojinasibu; Lakini sidhani kama alikuwa anajuwa hata changamoto ya ada yangu ya shule.

Acheni huu upuuzi wa kujazana ujinga, yaani wewe sister duh halafu hata ukujua wa kumchanulia kuja kutuandikia ujinga hapa with your struggles,
 
Back
Top Bottom