Hivi inawezekanaje mtu huna kazi bado unasoma Master's Degree?

Sisi wengine second degree tulienda kusoma sababu ya passion ❤️😍
 
Unaposoma ni elimu ikusaidie kuishi kwa kuweza kutatua changamoto za wasiosoma. Mkisoma alafu mnarudi mtaani kulia na ambao hawakusoma ni fedheha. Someni mpate elimu....elimu ni nzuri.
Elimu ni nzuri kama pesa unazo nje ya hapo ni kujilisha upepo. Utawaamkia hadi wadogo zako siku moja na hizo elimu zako ukiwa hela huna 🤣
 
Usomi hauna mwisho. Soma soma soma...
Kama hauko busy na idle, soma vitabu soma tu, why not?!
 
Elimu ni nzuri kama pesa unazo nje ya hapo ni kujilisha upepo. Utawaamkia hadi wadogo zako siku moja na hizo elimu zako ukiwa hela huna 🤣
Unadhani kwanini wanasiasa wengi wanakimbilia degree za mchongo....kwamba hawana hela? Elimu ina nafasi yake hata kama utawaamkia wadogo zako,kuna namna utawasalimia kisomi
 
Unadhani kwanini wanasiasa wengi wanakimbilia degree za mchongo....kwamba hawana hela? Elimu ina nafasi yake hata kama utawaamkia wadogo zako,kuna namna utawasalimia kisomi
Wanafanya hvo ili kulamba teuzi tu

Nje na hapo huwezi kuta wanazihangaikia

Sasa wewe huna mbele wala nyuma unafukuzia mi masters ya nini
 
Mlima mpaka wakome.
Ila najua wapo manunda watasema kusoma sana ni ufala.
Na mimi kupitia mtazamo wao huo kila mara nitakuwa wale wazee wakujitapa mbele zao hasa nikiwa nimewaacha mbali
Hongera mkuu elimu ni nzuri...na mimi hii yangu ya form siksi kuna wakati ilinipa shavu katikati ya kundi la wajinga na sikuamini. Katu sitoidharau elimu. Mungu nisaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…