Shida yetu watanzania tumeshakariri kwamba Tunaenda Shule Tusome ili tuje Tuajiriwe.
Nani katuharibu? Elimu imewekwa mtu aipate aondoe ujinga na wala sio ili amalize aajiriwe.
Ajira ni sehemu ndogo sana ambayo inapatikana kwa wenye elimu lakini Ajira sio kigezo cha Maana ya Elimu.
Soma ondoa Ujinga,Ongeza maarifa, Fahamu vitu ukimaliza, ingia duniani anza kukaanga vitumbua,kufanya usafi,boda boda,nk.
Hiyo ndio maana halisi ya Elimu, lakini hatusomi ili tukimaliza Tuajiriwe, Tulikua tukifahamu hivyo zamani lakini sasa tumeshaelewa na kutambua kwamba Elimu sio Ajira.
Hata kazi nyingine zinahitaji watu wenye elimu, Boda Boda wote wangekua na Elimu Ajali zisingekua kama zilizopo.
Mama ntilie wote wangekua na Elimu tusingepikiwa Wali marage kila Kibanda,nk nk.
Tuna ihifaji elimu itusaidie kuendesha maisha yetu kama wasomi kwa ubora sio Elimu itupe Ajira (kuajiriwa).