Hivi inawezekanaje mtu huna kazi bado unasoma Master's Degree?

Nimemuonya shemeji yangu amemaliza digrii ya public administration akakaa mtaani kujaribu kufuga kuku ameshindwa eti Sasa anamrubuni Mzee atoe kibunda Cha korosho akasome masters ! Akili zinatoka mbali sana
 
Kama ana Degree ya Accountancy asome CPA hiyo CPA ni marketable than masters
Kama ana Degree ya Law ni Bora asome law school awe Wakili,
Wote wanasota tu, cpa, masters, degree. Graduate asiye na bahati ya kazi na hana uwezo wa kujiajiri kwa kiwango cha elimu yake hata umpe level gani ya elimu haitampa kipato.
 
Au mtu anatoka 1st Degree anaunganisha na Masters.

Sasa sijui anaenda kusoma kumaster kitu gani.
 
Unajua hakuna mtu mwenye uhakika kwamba akifanya nini atafanikiwa. Kila mtu anajaribu. Kuna watu drs la saba wana mafanikio kuna drs la saba ni mafukara wa kutupwa. Kuna mtu masters ndo imempa +advantage akapata kazi nzuri kuna mtu diploma ndo imempa kazi nzuri.

Jamani. KILA MTU APAMBANE KWA LILE AMBALO ANAONA LINAWEZA KUMPA MAISHA ANAYOYATAKA, TUSIWE WACHAWI KUKAA NA KUTAFUTA WANAOKOSEA MAISHA TUWAITE WAJINGA. MAISHA HAYANA NJIA YA UHAKIKA YA MAFANIKIO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…