Hivi inawezekanaje mtu huna kazi bado unasoma Master's Degree?

Kuelimika na nini haswa?

Maana ukitaka kujielimisha kila kitu kipo mtandaoni.

Hata huko vyuoni unapodai una elimishwa, Huyo mwalimu anaye kuelimisha anatoa vitu mtandaoni.
Leo ukitaka kujielimisha chochote hapa Duniani kiko mtandaoni, sasa hawa wanaosema kuelimika ni kwenda kusoma master's degree ndio siwaelewi.
 
Hayakuhusu hangaika na maisha Yako

Huwezi moangia mtu Hela yake aitumiaje

Hela Yao wewe kinakuuma Nini ? Acha umbeya
Rudi shule ujifunze kuandika vizuri wewe kima.

Nyie ndio mnasoma master's degree kuelimika huku hata kuandika hamjui.

Darasa la 4 ulifaulu vipi na uandishi wa hivi?
 
Nakazia
 
Shida inakuja efficiency ya kazi kwa wasomi ni ndogo pia.
 
Shida yetu watanzania tumeshakariri kwamba Tunaenda Shule Tusome ili tuje Tuajiriwe.

Nani katuharibu? Elimu imewekwa mtu aipate aondoe ujinga na wala sio ili amalize aajiriwe.

Ajira ni sehemu ndogo sana ambayo inapatikana kwa wenye elimu lakini Ajira sio kigezo cha Maana ya Elimu.

Soma ondoa Ujinga,Ongeza maarifa, Fahamu vitu ukimaliza, ingia duniani anza kukaanga vitumbua,kufanya usafi,boda boda,nk.

Hiyo ndio maana halisi ya Elimu, lakini hatusomi ili tukimaliza Tuajiriwe, Tulikua tukifahamu hivyo zamani lakini sasa tumeshaelewa na kutambua kwamba Elimu sio Ajira.

Hata kazi nyingine zinahitaji watu wenye elimu, Boda Boda wote wangekua na Elimu Ajali zisingekua kama zilizopo.

Mama ntilie wote wangekua na Elimu tusingepikiwa Wali marage kila Kibanda,nk nk.

Tuna ihifaji elimu itusaidie kuendesha maisha yetu kama wasomi kwa ubora sio Elimu itupe Ajira (kuajiriwa).
 
Ukisoma ili uje uajiriwe ndio yale unasoma ili ufaulu automaticaly utajikuta unasoma kukariri na sio kuelewa maana hufati kinachotakiwa darsani unafata akili yako ilivyoji set. Ufaulu uajiriwe

usipoajiriwa unaanza laumu elimu haina maana as if hapo ulipo ni sawa na ulivyokua kabla ya kuipata elimu.

Tuwaze kwa angle nyingine matumizi ya elimu yetu tuachane na eneo la Ajira tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…