manchoso
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 1,605
- 2,055
Wamesema kweli wahenga
Baniani mbaya kiatu chake dawa na kiingiacho mjini si haramu
Corona sio siri imeleta majanga hakuna kinachofanyika kwa ufanisi, sio biashara siasa wala burudani kila mtu analia kimya kimya
Pia corona imetupa funzo darasa la bure lenye maumivu ndani yake ambalo bila shaka tutawahadithia wajukuu na vizazi vijavyo
Wale waponda mali na waliojinasibu kwamba wanakula ujana wanapata funzo kwamba starehe ziwe na mipaka ikumbuke kesho yako na akiba haiozi
Na nadhani corona imetusaidia pia kufanya meditation, kuifikiria na kuiona dunia katika uhalisia wake na asiye jifunza ajifunze kwamba sisi binaadamu si chochote ni dhaifu kirusi kidogo kinatuendesha mbio
Japokuwa wanasema sayansi ilipoishia ndo uchawi unaanzia lakini kwa corona naona imejua kuwanyoosha watu, zile kelele za usiku za mapaka pia zimepungua sana siku hizi,hivi walozi wakimgusa mtu mwenye corona wanapata maambukizi???