Hivi kama mkuu wa usalama anahusishwa na na kashfa za ufisadi wa kupindukia, tunaweza sema bado tuna nchi?

Hivi kama mkuu wa usalama anahusishwa na na kashfa za ufisadi wa kupindukia, tunaweza sema bado tuna nchi?

Kila nikikaa kufikiria Tanzania aseeh roho unaniuma kiasi cha kutokwa na machozi.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu wabariki wananchi wa Tanzania.
 
Mombo alitupwa ubalozini huko kipindi Cha mwendazake. Sababu ya kumrudisha aulizwe mwanamtandao nchimbi.

"Ni kama nchi HAINA mwenyewe" Polepole
 
Kibaya zaidi mwanae anaonyesha dole la kati hata maadili kidogo baba mtu ameshindwa ataweza kusimamia maadili na maslahi ya nchi
Hapo inaonyesha malezi ni ya hovyo...
Ujue familia yako kama baba kwa asilimia kubwa ina reflect malezi, utu na tabia zako...

Ingekuwa mtoto wa Kajamba nani ungesikia anatafutwa na kupewa kesi ya matumizi mabaya ya mtandao...
 
Ni hao wazalendo na waadilifu ndo wale hata kule Russia walimfuata na waliongea na raisi Boris Yeltsin kumpa jina la mtu walieona afaa kuongoza taasisi ya usalama kisha wakamfuata Putin ambae alikuwa zake vekesheni Tuscany, Italy baada ya kupiga kazi ya maana kule Ujerumani mashariki.

Huko wakampa blueprint na tangia pale baas, hadi leo jamaa yupo akiweka order na kuzunguruka Duniani bila shida.
una uhakika ni wazalendo na waadilifu walimuweka putin madarakani? unajua uhusiano wa mtoto pekee wa boris (tatyana) na roman abramovic? unajua kuhusu alminium war? unajua kuhusu visima vya mafuta vya russia na vita yake? unamfahamu mshika mfuko wa fedha wa wazee wa kremlin? Unafahamu kuhusu maoligarch wa kremlin, unafahamu ukaribu wa putin na oligarch roman abramovich aka mr A?
 
Sina maana hiyo mama utaniua maana yangu ni hii huyu DG wa Tiss kuna kipindi tuliambiwa amekufa wanamzika Tanga Je kama ni propaganda za wale waliokua wameeneza habari za yeye kufa wanamtengenezea ajali atoke hapo kwenye UDG mimi nakua na mawazo huru. Ila nakupenda sana😂😂
😂😂😂😂
 
Wakuu mimi kuna kitu bado sielewi, hivi inawezekana vipi huyu mtu kuwa na kashfa mpaka watoto wake kuanikwa hadharani anaweza vipi kulinda maslahi mapana ya nchi?

Kama yeye yuko hivyo vipi hao wa chini yake hali ikoje? Ina maana huko idarani ndo kumeoza kabisa kwa viwango hivi? Hivi bado tunaweza simama na kusema bado tuna taifa au ndo tushafika viwango kamili vya "Failed State"?
Tukisema tunatekwa
 
Back
Top Bottom