GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,685
- 128,178
Na je, unadhani kama Yeye Boss wao yuko hivyo Watendaji wake nao wataacha Kumuiga? Na je, kama hali ndiyo iko hivi tunaweza Kujiaminisha sasa kuwa nchi iko salama kwa Adui wa ndani na wa nje. Bado kwangu Mimi idara bora za Usalama wa Taifa kuwahi kutokea ni ile ya Mwalimu Nyerere na ya Mkapa ila ya Mwinyi ilianza Kulegalega kabla haijapata Msaada wa Kiuzoefu (hasa wa Kimaadili) kutoka kwa ile ya Mwalimu Nyerere.Wakuu mimi kuna kitu bado sielewi, hivi inawezekana vipi huyu mtu kuwa na kashfa mpaka watoto wake kuanikwa hadharani anaweza vipi kulinda maslahi mapana ya nchi?
Kama yeye yuko hivyo vipi hao wa chini yake hali ikoje? Ina maana huko idarani ndo kumeoza kabisa kwa viwango hivi? Hivi bado tunaweza simama na kusema bado tuna taifa au ndo tushafika viwango kamili vya "Failed State"?
Ila Idara hii ilianza Kuharibika hasa na pakubwa katika Awamu ya Kikwete na ikaja Kurithiwa na ya Magufuli ila hii ya sasa nadhani ndiyo Funga Kazi. Bado idara ina Watendaji Waadilifu na wenye Uzalendo wa kweli, lakini tatizo ni kwamba Wamemezwa na Kundi fulani ndani yao lenye Ushawishi kwa Kiongozi wa nchi hivyo hawa Waadilifu na Wazalendo wakisema wapaze Sauti zao ili kuirejesha Idara ya Usalama wa Taifa mahala pake wanaonekana ama Maadui au Wasaliti katika kuhakikisha Ufisadi unaendelea kwa Mabosi zao. Inasikitisha sana na kuogopesha mno hasa ukiwa ni mfuatiliaji wa Masuala mazima ya Usalama Duniani.