Hivi kati ya kuwa msomi na mfanyabiashara ni yupi ana advantage kubwa katika maisha ??!

Hivi kati ya kuwa msomi na mfanyabiashara ni yupi ana advantage kubwa katika maisha ??!

Jibu ni mfabiashara ndugu wala mtu asikudanganye.
1. Ukiwa mfanya biashara ndio unaweza kuwa tajiri
2. Unaweza kuwa maarufu
3. Unaweza kuajiri watu wakufanyie kazi huku wewe umekaa nyumbani
Wewe mwenyewe unajionea mtaani jinsi wafanya biashara wanavyo ishi maisha ya uhuru huku wafanyakazi wakiwa busy muda wote na utumwa.
Asikudanganye mtu msomi mfanyakazi ni mtumwa aliye changamka.
 
Mafanikio ni wewe na akili yako,mipango yako na nidhamu yako,haijalishi uko wapi,

Ndio maana hata nchi tajiri wapo masikini pia,na kwenye nchi masikini wapo matajiri pia,

Elimu ni elimu tu huwezi kuifananisha na vitu vingine,kila kitu kinaanza na elimu,
Elimu sio tu ile unayo fundishwa darasani,

Ukiwa mfanyabiashara mkubwa ni lazima utawahitaji/utaajiri wenye elimu ili wakusaidie,utahitaji vifaa vya kufanyia kazi,kama vile computer,Internet,meza,viti,kabati,usafiri,vitu ambavyo tunavyo leo hii kutokana na matokeo ya elimu,hata jengo la ofisi yako limejengwa na wataalamu wenye elimu,

Mleta mada ungeuliza kati ya muajiriwa na mfanya biashara na sio kati ya msomi na mfanyabiashara,Elimu sio lazima iwe ile uliyoipata darasani.
 
Back
Top Bottom