Hivi kuandika hivi Kwa kizazi hiki ndio swaga ama Nini?

Sasa ukishinda nao unawasikiliza bila kuchangia au unakuwa mwanafunzi ukipewa somo😁
Hao ili muendane usiwe mchangiaji sana maana utaharibu utaanza kuongea vitu vya 47 wakati wenziyo wapo 2026 .
Hapo ni kuwa msikilizaji ila zaidi unakuwa kasponsor kadogo walau tubia ni hapo tunakuzoea haraka siku unakuta tunakuonesha na mdada yeyote mara vipi pale mzee tukukalishe ? 😀😀

Unabaki kutoa macho tu kikongwe wa watu ,utafanyaje ndiyo utandawqzi wenyewe
 
Hebu usinichekeshe mkwee🤣🤣🤣

Na kweli tuna tabia za namna hiyo ukikanunulia hata henessy pori tu aisee kanakuwa chawa ghafla, mimi kijqnq wangu nashindwaga hata kumjibu utasikia tu oyaa sistaa..! Huwa nacheka😆
 
Hebu usinichekeshe mkwee🤣🤣🤣

Na kweli tuna tabia za namna hiyo ukikanunulia hata henessy pori tu aisee kanakuwa chawa ghafla, mimi kijqnq wangu nashindwaga hata kumjibu utasikia tu oyaa sistaa..! Huwa nacheka😆
Tunafurahisha sana tutoto twa kileo kengine siku kananiuliza eti kwani mshua master ilikuwaje mpaka shemeji akakubwaga ?

Hapo eti nikape sababu kanataka kunishauri nikabaki nachekea moyoni kuwa sasa kukaa nako meza moja tukavuruga akili sasa kanajiona kanaweza kunishauri ,nikakambia wewe bado mdogo mwanangu tunywe pombe kesho ukiwa sawa nitakuambia ,kesho nakakumbusha kanasema utoto huu nitakushauri nini boss wangu .

Yaani tafrani tupu
 
Eti mshua master🤣
Yani umenichekesha..ona huyu sasa🤣 wana vituko hawa vijana wa kisasa🙌🏾
 
Eti mshua master🤣
Yani umenichekesha..View attachment 3564579ona huyu sasa🤣 wana vituko hawa vijana wa kisasa🙌🏾
Wana maneno yao fulani ukiwa mgeni huwezi kuwaelewa kabisa ,kuitwa mshua master hapo kuna kitu au vitu vingi kanaviadmire kwako ila ukiitwa father ,mara dingi au mkola jua tumeshakuona wewe safari yako ina mabonde mengi sana huko mbeleni kufikia lengo lako
 
Tena??😂 afadhali sijawahi kuitwa maza au bi mkubwa ningekoma😁

Siku moja alipita dada mmoja mrefu halafu ana ziwa, yani pande la mdada! Basi kijana akaropoka cheki hilo lidada sistaa lina bonge ya mbavuu🤣 nilicheka duhh, sijui wanatoa wapi maneno! Mi nawakubali ukiwanununulia hata jobo tu wanakushukuru sana🙌🏾
 
Nisiwe muongo hii ndiyo kampani ninayoenjoy zaidi maana natoa stress za kukaa na vizee vyenzangu ,maana ukikaa navyo mara kidogo kimpigie mkewe mara akiulize habari za usiku tunakula nini ,mara kuku hawajurudi bandani ,sasa lazima akusimulie wakati huo mimi sitaki kusikia yasiyonihusu ikiwa sitaongozana na wewe kwenda kula kwako .

Ila hutu tutoto unaweza kukesha nao bar hutosikia sijui nyumbani ,sijui nini ila kikubwa asubhi ukubali kuombwa hela ya supu na kutudrive mpaka mitaa yao .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…