Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,315
- 104,500
Uko sahihi mkwe! Kuna kundi ukiongozana nalo pia unafiki wivu na magomvi yakipuuzi! Bora umechagua kakundi ka madogo hapo huwezi kuonewa wivu, huwezi kusikia hili wala lile! Hao hawana pressure unaishi nao kama wanao tu, uzuri watakuheshimu na kuwa machawa hata ukiwa na kadem kazinguaji wanakusanua mapemaa😁Nisiwe muongo hii ndiyo kampani ninayoenjoy zaidi maana natoa stress za kukaa na vizee vyenzangu ,maana ukikaa navyo mara kidogo kimpigie mkewe mara akiulize habari za usiku tunakula nini ,mara kuku hawajurudi bandani ,sasa lazima akusimulie wakati huo mimi sitaki kusikia yasiyonihusu ikiwa sitaongozana na wewe kwenda kula kwako .
Ila hutu tutoto unaweza kukesha nao bar hutosikia sijui nyumbani ,sijui nini ila kikubwa asubhi ukubali kuombwa hela ya supu na kutudrive mpaka mitaa yao .