Kitu nilichojifunza kwenye huu uzi wana JF wameongea uhalisia wa maisha yao, kule kwwnye nyuzi nyingine ukizisoma unaweza ukafikiri kila mwana JF anamiliki ndinga la kuanzia milionj 50..
Anyway, nirudi kwenye point...ni kweli ukiwasha gari uwe na akiba yoyoye mfukoni mathalani elfu 10 kwenda juu....na hii elfu kumi tafuta change kabisa za buku buku....unaweza kunasa hata kweny katope watoto wa kitaa wakakupush wakakudai hata buku 2,
kama huna hizo buku 2 utapewa maneno ya shombo kama mchuzi wa bata..
Lakini pia, tuwe tunatabia ya kumuomba mungu atuepushe na majanga ya ajali huko bara barani kwa sababu gari ni tatizo linalotembea..
Linaweza kugonga gari la mwenzako, ukalipa.
Linaweza likagonga ukuta wa nyumba ya mtu, ukamjengea
Linaweza kugonga mtu, ukamtibu au ukagharamia mazishi..
Linaweza kukupatia ajali ukapata ulemavu..
Hivyo tumtangulize Mungu tunapoendesha hivi vyombo..
Ni hayo tu WAJUMBE