Mkuu ulikaa na wasukuma wa wapi?
Maana wasukuma wanapatikana katika mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Simiyu,Tabora na kwa sasa wameukamata mkoa wa Katavi.
Na kila mkoa wana viutamaduni vyao vidogovidogo vinavyowatofautisha na mkoa mwingine mf namna ya kuongea pengine na aina ya maisha.
Wasukuma wa Mwanza ni tofauti kabisa na wale wa Tabora japo wote ni wasukuma.
Wale wa Simiyu pia wana maneno yao ambayo ni mara chache kuyasikia Tabora na Mwanza.
Sasa ukisemea roho mbaya kwa wasukuma sijui unakuwa unazungumzia msukuma wa wapi tu,maana sisi Mwanza unaweza kwenda kwenye mji wowote ukaomba kupikiwa chakula na ukala bila shida,mashamba haya zamani wasiokuwa nayo unapewa tu kulima kwa wale wasiokuwa na mashamba ya kutosha na hamna shida kabisa,ubaguzi wa makabila mengine hakuna kabisa cha msingi jitahidi tu ujue lugha yao japo kidogo itakusaidia sana kupata unachokitaka maana wana utaratibu wa kumpuuza asiyejua wana ile hali ya kuamini kila mtu anajua tu kisukuma.