Hivi kuna mantiki ya wanamichezo kuvaa vichupi kwenye Olympic

Hivi kuna mantiki ya wanamichezo kuvaa vichupi kwenye Olympic

Mchezo kama ule wa gymnastics unawezekana kweli mtu akivaa hijab huku kafunika uso
 
Nilienjoy sana kuliangalia lile shindano...Mungu fundi kwakweli
Mimi niliangalia session zote 2 mwanzo mwisho, kwakweli lilikuwa zuri sana hadi akashinda yule Sofia Raffaeli.

Nimeangalia ratiba hapa naona leo pia lipo ila ni kwa magroup, na kesho pia.
 
sijaona umuhimu kabisa hata wa ile michezo imagine mtu anaenda kulenga kibastola...yani utoto ni mwingi kweli sometimes unatakiwa ujitoe akili ili uishi.

Inapaswa michezo yote tuipe Uzito ili ajira ziwe nyingi.
Mashindano Yako mengi ambayo kwa Mshindi wa Gold anakunja kitita cha hela isiyo pungia 60Milioni ya kitanzania.
Jee hela kama hizo tukiwategeneza vijawa wetu wakazipata unahisi tumeokoa familia ngapi .
Alafu ukiwa nje utaona ni simple sana ila Science, umakini na kipaji ndo kinaweza mtu kushinda.

Tatizo sisi tumeweka tuu akili kwenye mpira tena wa vilabu peke yake na ukitizama wachezaji wazuri wanatoka njee. I
Huku Idadi ya watu inaenda kufika miliomi 65.
Ndo matatizo ya ajira yanapoanzia hapa.
 
Hata wakina kaka pia wanavaa vichupi
 

Attachments

  • Screenshot_20240807_233220_Facebook.jpg
    Screenshot_20240807_233220_Facebook.jpg
    162.9 KB · Views: 5
Back
Top Bottom