Nimeishi mikoa zaidi ya 8 hapa Bongo ila hakuna mkoa ulijua kuninyoosha kama Mbeya.
Nakumbuka mara yangu ya kwanza kabisa kufika 2018 iyo nilikaa Lodge kama wiki hivi nikitafuta Chumba cha kuishi nikabahatika kupata maeneo ya Checkpoint-Forest ya Zamani huwezi amini baada ya wiki tu nikaibiwa simu 3, Laptop na Wallet ilokua na akiba yangu yote pamoja na vitambulisho aisee sijawahi kuvurugwa kichwa kama iyo siku kwenye maisha yangu tangu nizaliwe. Nilikua naishi karibu na ofisi ya RPC ikabidi niende kuripoti apo nikaambiwa inabidi niende Central Police kule Letco na apo sina ata mia mbovu nikatembea mpaka kituoni nikaripoti lkn sikuambulia msaada wowote zaidi ya kunitia hasara ya kuandika Lost Reports. tangu iyo siku niliacha kuripoti kitu polisi.
Mara ya pili 2020 narudi kutoka likizo nakuta Geto jeupeeeeee hahaah, Hii awamu ndo walinikomesha kabisa. walihamisha kila kitu pamoja na vyeti vyangu vyote vya elimu kuanzia Darasa la Saba mpaka Form 6. kuulizia majirani wananambia kuna mkaka walikua wanamuona anaishi apo wakajua labda tunajuana aliwaambia kuwa tunahamia sehemu nyingine aisee niliishiwa Nguvu ikabidi nikaishi kwa Dem wangu kwa muda.
hayo matukio Mbeya ni kawaida sana hasa mitaa ya Forest. Mbeya ni mkoa ambao huwa siwezi kuusahau kwenye Maisha yangu. Salute 🫡