Hivi kuna mkoa unaongoza kwa wizi wa kusafisha Nyumba nzima kama Mbeya?

Hivi kuna mkoa unaongoza kwa wizi wa kusafisha Nyumba nzima kama Mbeya?

Anaekuibia hatoki mbali. Anajua ratiba zako zote. Pole sana najua maumivu yake.
The feeling mtu alikuwa ndani kwako ina depress.
Acha tu....Niliumia...

Na waliingia mchana nipo kazini....Wakachukua walichochukua hadi mboksi na Remote zake...
Wakachukua na simu....Nadhani walishtuka wakaona simu itasababisha wakamatwe Wakairudisha baada ya siku mbili..Asubuhi tunaikuta imetupwa kibarazani😭
 
Tukiwa wadogo mama alikuwa anatusimulia kuwa kuna mwizi aliwahi kutokea hiyo Mbeya, aliitwa Mwamikubha yeye pia alikuwa anakuibia kila kitu ndani.
Hata akiamua kukuibia nguo ulizovaa, unaamka asubuhi uko uchi.

Unaambiwa jamaa alikuwa na dawa akiwawekeeni nyote mnalala usingizi wa kifo nyumba nzima ndo anawapukutisha.

Alikuwa na dawa nyingine anakuotesha ndoto, unaota unasafiri, unaanza kutoa vitu nje ukiwa kwenye hali ya usingizi, ukimaliza unaingia ndani unalala, anasomba mazaga yote anatembea.
 
sishangai, ushawahi kusikia wizi wa kuzubaishwa? yani akili yako ikijirudi unajikuta huna chochote na niwewe mwenyewe umempa mwizi? sasa Mbeya ndo nyumbani
 
Acha tu....Niliumia...

Na waliingia mchana nipo kazini....Wakachukua walichochukua hadi mboksi na Remote zake...
Wakachukua na simu....Nadhani walishtuka wakaona simu itasababisha wakamatwe Wakairudisha baada ya siku mbili..Asubuhi tunaikuta imetupwa kibarazani😭
Pole sana.
 
Hayo makitu hamna kitu ni uongo. Jinsi watu walivyo na hasira na wezi yangekuwa yanafanya kazi basi hakuna mwizi angeachwa aendelee kuiba maisha yake yote.
Aisee mimi nitatafuta tuu huko kwa wasukuma ndani ndani, yaani nitatumia gharama hata zaidi ya walichoniibia niwakomeshe. Maisha magumu alafu mtu anavunja kwako haupo anakusafishia vyote unarudi unakuta tambala la deki.
 
mkuu nilipokua naishi ni dakika moja tu nipo kwa RPC, dakika 3 nipo mahakama kuu na Nyumba za jirani walikua wanaishi Askari ukisogea mbele kidogo alikua anaishi Mkuu wa Askari Upelelezi Mbeya licha ya ivo Mkuu wa Mkoa alikua anapenda sana kuja huo mtaa kwa mchepuko wake lakini ndo mtaa ulikua unaongoza kwa watu kusafishiwa nyumba
Nilikaa mtaa huo pia...waliiba kila kitu...nashukuru Mungu nilikua na pesa ya kuwalipa per diem watu niliokuwa nawafanyia training niliviringisha kwenye tambara bovu na laptop wakati nikitoka so hawakuiba ila walibeba kila kitu! Wakarudi siku nyingine nikiwa nimesafiri ,walikuja na bajaji, majirani wakakamata mmoja na bajaji aisee
 
Nimeishi mikoa zaidi ya 8 hapa Bongo ila hakuna mkoa ulijua kuninyoosha kama Mbeya.

Nakumbuka mara yangu ya kwanza kabisa kufika 2018 iyo nilikaa Lodge kama wiki hivi nikitafuta Chumba cha kuishi nikabahatika kupata maeneo ya Checkpoint-Forest ya Zamani huwezi amini baada ya wiki tu nikaibiwa simu 3, Laptop na Wallet ilokua na akiba yangu yote pamoja na vitambulisho aisee sijawahi kuvurugwa kichwa kama iyo siku kwenye maisha yangu tangu nizaliwe. Nilikua naishi karibu na ofisi ya RPC ikabidi niende kuripoti apo nikaambiwa inabidi niende Central Police kule Letco na apo sina ata mia mbovu nikatembea mpaka kituoni nikaripoti lkn sikuambulia msaada wowote zaidi ya kunitia hasara ya kuandika Lost Reports. tangu iyo siku niliacha kuripoti kitu polisi.

Mara ya pili 2020 narudi kutoka likizo nakuta Geto jeupeeeeee hahaah, Hii awamu ndo walinikomesha kabisa. walihamisha kila kitu pamoja na vyeti vyangu vyote vya elimu kuanzia Darasa la Saba mpaka Form 6. kuulizia majirani wananambia kuna mkaka walikua wanamuona anaishi apo wakajua labda tunajuana aliwaambia kuwa tunahamia sehemu nyingine aisee niliishiwa Nguvu ikabidi nikaishi kwa Dem wangu kwa muda.

hayo matukio Mbeya ni kawaida sana hasa mitaa ya Forest. Mbeya ni mkoa ambao huwa siwezi kuusahau kwenye Maisha yangu. Salute 🫡
Iringa, kihesa walinisafisha kila kitu mbwa wale.
 
Back
Top Bottom