Hivi kuna perfume ya kiume yenye kunukia vizuri kuliko hii?

Mwanaume unajipaka perfume umekuwa maiti?
 
Bado parefu sana
Huko juu nimetaja perfume zangu mbili pendwa hazizidi 27K Royale Blue na Romance hazi. Nikiwa sina pesa kabisa Everyone ingawa siku hizi wameichakachua lakini inaniondolea harufu ya kwapa
 
Tangazo la kitalaam Sana hili
 
Mtoa mada kuna watu watakuuliza unapaka perfume ya laki 3 unapanda mwendokasi 🀣
 
Perfume nzuri sana hii nakumbuka niliwahi pewa kama zawadi na demu wangu mtoto wa waziri kwa kipindi hicho nlishindwa kuendelea nayo sababu ya kipato, But soon nafikiri nianze kuitumia tena
 
Mwanaume usipake hata mafuta
Dume zima limevaa macheni shingoni kama minyororo ya KUFUNGUA Mbwa, mikononi mafurushi ya mipete, meno limeweka coating za silver halafu limejimwagia manukato kama ya kuzikia maiti linapita barabarani ? Hovyo kabisa
 
pafyumu laki 3 na ushee alafu unapanda mwendokasi kuna kitu mahali hakipo sawa
Mkuu parfum ni kama nguo,,so unapoivaa mwilini ni kama umevaa nguo fulani special.

Ni vzr uvae yenye thamani kubwa ili ilinde confidence yako.

Kutembea kwa mguu sio kigezo cha kufanya ushindwe kumiliki parfum ya bei ghali..
Kujipenda ni tabia kama zilivyo tabia zingine za mwanadamu mfano ulevi nk.

Wapo watu wanaendesha magari ya thamani lakini akikupitia karibu ni kama beberu la mbuzi kwa harufu .
Na yupo mtu anatembea kwa mguu lakinj very good looking and smells good.
 
Achana nae huyo.. feki yake ipo Tsh 35,000 tu na huwezi jua tofauti πŸ˜€
First of all perfume ikishakuwa chini ya 100,000/= hiyo tena siyo pafum hayo ni maji na zaidi sana amini mkuu,original ni original tu anayetumia original na anayetumia fake wakikatiza mahali wa original atajiamini zaidi kuliko wa fake.

Any way,tuendelee kufarijiana huku tukiendelea kupambana kuongeza kipato siku na sisi tununue hizo za malaki kama siyo mamilioni.
 
Mi mpaka leo sijuagi sijui perfume ya kiume sijui ya kike .

An me yoyote ile napita nayo...
 
Ah bana we.. sasa kama unatumia perfume ya laki 4 halafu hamna mtu anaejua kama perfume yako ni ya ghali hayo si matumizi mabaya ya hela..?

Raha ya kitu cha ghali ni watu wajueπŸ˜„ Kama lengo ni kunukia tuu mbona hata hizi za 35k zinanukia vizuri tena zinakaa kwenye nguo kutwa nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…