ETI 'JENZII' MREMBO ALITIA NENO KWA RC (MKUU WA MKOA) WA TABORA!
Ni kati ya mwaka 1380 na 1050 Kabla ya Kristo wakati huo Ruth alifiwa na mumewe. Lakini mama mkwe wa Ruth, aliyeitwa Naomi aliona kuwa isingekuwa vema mkwe wake aendelee kuwa mjane. Akampatia mbinu ya kujipitisha kwa Boaz.
Alijipitisha hadi Boaz akaamua kumuoa Ruth. Ruth na Boaz wakamzaa Obed, Obed akamzaa Yese na Yese akamzaa Daudi (Ruth 4:18-22). Yesu alitokea ukoo wa Daudi (Mathayo 1:1-17). Unaweza kusoma kisa kizima cha huyo 'Jenzii mrembo' aliyetia neno kwa Boaz!
Sijui dini na imani ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Lakini angekuwa ni Mkristo pengine angejua kuwa yeye hakuwa mtu wa kwanza pia kutakiwa na mwanamke na hivyo asingetumia muda na rasilimali zetu kumtumia Kamanda wa Polisi wa kumkoa husika kumhoji Sophia. Na huenda pia asingetumia vibaya rasilimali za nchi kwa kutaka mahakama isikilize kesi juu ya Sophia kumtaka yeye.
Lakini pia Mheshimiwa huyo angekuwa Mkristo asingeshangaa sana kwani hata Yesu alitakiwa na mwanamke aliyekuwa anateka maji katika kisima. Badala ya kuamuaibisha yule mrembo, Yesu alimsimulia habari za ufalme wa Mungu!
Lakini nchi yetu na dunia yetu haiishi kuwa na vituko. Natamani pia kusikia kesho kuambiwa kuwa hiyo fake news!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 8 Septemba 2026; Saa 2:20 usiku.