Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Maombi Yako yalikua Kelele Kwa Mungu, Mungu Huwa hasikilizi na kujibu maombi ya Aina hiyo.

Huyo Mtu hakufa Kwa sababu wewe uliomba afe.
Naamini hivyo pia,.
Apumzike kwa Amani
 
Serious aliniibia halafu akaninyima kufutia na wakanicheka yeye na wenzie ( Ilikuwa ni aibu🥲🥲)..

Japo kwa kuchelewa ila nimemsamehe na Roho yake ipumzike kwa amani
Ilitakiwa ukaze,hakuna kutoa msamaha kwa "maliyemu".Unavyotoa msamaha baada ya "marehemu kufa" inatuambia kwamba unaogopa kifo.Member wa JF unaogopaje kifo?😝😝😝😝
 
nowdays niko na wepesi wa kusamehe na kutake vitu easy,. nazani sijui ulikua ni utoto maana hadi nlikua nimeshamsahau yule binti
Pole aisee, Mimi huwa sipendi kuumiza mtu kwa vyovyote vile pia sipendagi kuonewa kabisa so Mimi huwa nawekaga fence sizoeleki na sina mazoea ya KIJINGA so ukinichokoza umemchokoza JOHN CENA.
 
Kama darasa la nne ulikuwa na uwezo wa kuombea wenzio mabaya, naamini kwasasa ushakuwa mchawi wewe.
Kabisa,na siku nilipoona anamkandia wastara kuombaomba msaada ingali yupo serious kitandani...nikajisemea,duh,moyo wa binti huyu...mmh!
 
Hiyo ni lesso na kiatu kimoja kubaki na vumbi,je ungeuliwa mzazi sijui ungekuwaje,ungetamani dunia yote tufe
 
Wakuu habari za kuamka....

Mwenzenu najiskia vibaya sana sana sana yaani vibaya mnooo.. Natamani hata nisingekua nimeshika simu leo,. Kuna mtu kaweka status "Forever in our hearts" kampost mtu ambaye alifariki 2012 hadi nilishamsahau,. Nilikua mtoto lakini huyu mtu kila siku nilikua namuombea kwa Mungu afe,.

Ilikua hivi,. Nakumbuka Kabla ya likizo ya pasaka nlikua darasa la nne by then.. Tulikua tunafanya mitihani ya Joint shule nyingi nyingi na wale wanaokuwa topten mnaitwa mnapewa zawadi mnashangiliwa na kombe mnapewa kurudi nalo shuleni

Hiyo siku na mimi nilipass nikawa nominated kati ya ambao wataenda kuchukua zawadi,. Mda tunajiandaa tukaanza kujisafisha yaani kama kufuta viatu, kujiweka tu vizuri, nikatafuta lesso yangu nifutie viatu sikuiona.. Huyu binti ambae ni marehemu Alitoa lesso watu wote wakawa wamefutia viatu mimi nlikua wa mwisho ikafika zamu yangu huku najifuta nikaangalia vizuri nikaijua ni lesso yangu ambayo nlikua naitafuta, nikamwambia hii mbona lesso yangu nlikua naitafuta umeipata wapi? Si akakasirika akaninyang' anya nikamwambia basi nikupa iwe yako niachie tu nimalizie kufutia maana ndio nlikua nimeitwa niende mbele Akagoma .

Imagine nimeenda Mbele yatu wengi wanafunzi wa karibia shule 10 na walimu ,kiatu kimoja kisafi kingine kina Vumbi halafu yeye na rafiki zake walikua wananicheka 😭😭😭,. Ile siku hata sikuifurahia nilivyotoka tu nikapiga picha (na kiatu changu kimoja kina vumbi mwenyewe) nikarudi zangu nyumbani hata sikuongea na mtu...

To be honest tangu sikuile nilikua namchukia , mda wa kusali sala za jioni au asubuhi au kanisani nlikua namwambia Mungu kwanini watu wenye Roho mbaya unawaacha waishi,. Nlikua namwomba Mungu kila siku yule binti afe,. nilikua simpendi yaani kila siku nlikua namwambia Mungu huyu mtu asipokufa mimi nitaacha kusali maana ni anaroho mbaya kwanini asife tu?

Wakati tunakaribia kufunga shule December alianzaga kuumwa akawa na vidonda vidonda,nywele zake zilikua zinayonyoka Alikua anababuka midomo, Mara shuleni haji,. kwa wiki anaweza aje siku moja na akifika basi kuna mda anaanza kuumwa mara anatapika mzazi wake anakuja kumchukua, tulikua tunaambiwa Fulani anaumwa mkipata nafasi mkamwone me sikwenda hata siku moja, Kwanza nlikua nafurahi rohoni namwambia Mungu saizi ndio muda wake huu wa kufa, Wakati tupo darasa la tano alifariki nikawa najiskia amani kwanza hadi nilishamsahau... Tulikujaga tu kujua baadae kumbe alikua ni HIV POSITIVE tangu alivyozaliwa,.

Hapa nimekaa najiskia tu huzuni maybe hatakama alikua HIV positive pangine angeishi mda mrefu ila maombi yangu yalikuwa yanapigilia misumari mpaka akafa mwee!!,. Nimetoka kumwambia Mungu kama maombi yangu yalihusika anisamehe maana sikua najua nafanya nini kwa kipindi kile ni utoto tu😒🙏🙏

Ila sidhani kama maombi mabaya huwa yanaskilizwa🤔🤔
Kumbe we ndo mdogo hivyo, so now upo chuo kikuu mwaka wa tatu siyo.

Maombi ya kipindi hicho yalijaa utoto, Mungu hawezi kusikiliza maombi ya kitoto yasiyo na mantiki.
 
Hata mwenyezi Mungu ana hasira, ndiyo sababu mtenda dhambi anaadhibiwa
 
Natengua kila Agano, karma ana laana in Jesus name,. My mind reprogramed since way back.

Ni kwamba nilishamsahau zamani mno accidentally tu leo nimekumbuka tukio lake,. means Mungu ana makusudi kunikumbusha alitaka nitubu na nimefanya hivyo🙏🙏🙏

So, stop scaring me please😭
Don't be scared you can't erase ur bad karma for prayers .

What going around comes around.
 
Back
Top Bottom