Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Kweli mtihani uko hapa. Rais alishasema kuwa wapinzani ni kikwazo kwake. Sioni jinsi gani atapata ushirikiano toka kwa serikali
 
Huu mkosi mkubwa
Wenzio wamepitishwa bila kupingwa..
Wengine polisi wameingiza masanduku mradi wapite...

Sasa inakuaje chama kisimsaidie na yeye??
Nasikia wamemuambia Kessy atulie watampangia kazi nyingine. Nasikia pia kuna Waheshimiwa wengine kitoka kanda ile pendwa walioporwa ushindi wao, Jiwe ktk vile viti vyake atawachomeka japokuwa wanatokea kwa mama wa kambo.
 

Kwanini Aidan ajiuzulu ubunge? Yaani kwa sababu Mbowe kakosa na wote wakose? Yaani mnataka ule upumbavu wa Maalim alipokosa Urais akaamuru wawakilishi nao waaachie ngazi as a result wakati wote wa awamu ya pili ya Dr Shein bunge likawa halina mjumbe wa CUF?? Hii ndo tonaita ubinafsi, egoism, wivu, nimekosa kwa hiyo tukose wote!!!! Shame! Aidan endelea na kibarua chako usisikilize mjinga yeyote kutoka CHADEMA au ACT-Wazalendo.
 
Eti ndo wanajiita wanademokrasia! Wamvue uanachama aje ccm tutampitisha agombee tu!
 
Ccm watamzonga sana aunge juhudi,hii ni zuga tu ya NECccm.huyo mbunge inawezekekana wamemuchia sababu ni afisa kifichowao.
 
Eti ndo wanajiita wanademokrasia! Wamvue uanachama aje ccm tutampitisha agombee tu!
Kesy ataenda mahakamani kupinga matokeo na atashinda.
Baada ya hapo uchaguzi Mdogo utafanyika na kesi atarudishwa ubunge.
Kesy ana jukumu kubwa sana alilopewa na Ndugai ya kui raise ishu yakumuongezea mkulu muda Wa uongozi,so anahitajika sana bunge lijalo.
 
CHADEMA achane upumbavu na ubinafsi,huyu dada namfahamu tumewahi kuishi mtaa mmoja .
Mwanzoni ilitakiwa agombee sumbawanga mjini ila hakuwa na mahusiano mazur na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa.
Kpnd cha kampeni kapambana mwenyewe hakupata support ya chama ngazi ya mkoa .
Huyu dada anaushawishi All kessy wananchi walikuwa wamemchoka kitambo tu,Aida kaungwa mkono hasa ukanda wa mwambao wa ziwa Tanganyika yaani Kirando na Kabwe maana kule CHADEMA ina nguvu huyu kashinda kiuhalali kabisa hajabebwa.
Huu wivu wa kishetani sijui unatoka wapi.
Mkimtimua kwenye chama ili apoteze ubunge next election mtawaambia nn wananchi ili wawaelewe?
 
Hivi hawezi akampa hiko kijiti mwingine?

Au zile ofa za Jiwe hawezi pewa hapo ili sasa atetee?
 
Namshauri aende bungeni, afanye kazi na wenzake waccm kwa ukaribu kabisa, huku jimboni nako ahakikishe anashirikiana na wale wajumbe wale, ikifika 2025 aunge mkono juhudi, aombe ridha ya kurudi tena kupitia ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…