Hivi kwanini CCM huwa wanapendwa sehemu zisizokuwa na maendeleo?

Hivi kwanini CCM huwa wanapendwa sehemu zisizokuwa na maendeleo?

nadhani kati ya sababu ni mijadala kama hii inayoendelea, tunawatusi, tunawakejeli, tunawadharau, tunawashutumu, na hatutoi suluhisho kwao ...... Matusi yetu kwao, kejeli zetu kwao, dharau zetu kwao .....wao hutoa majibu kwenye sanduku la kura maana ndipo pekee wanapoweza kupaza sauti zao na kusikika...!
Vilevike nipendekeze jambo moja, ifike wakati tuache kuwadharau (japo pengine huonekana ni hali halisi) na kuonyesha tupo pamoja nao ktk shida zao ....tufanye kwa vitendo na si maneno matupu, .... Katika "say" wilaya ama tarafa nzima ambayo maendeleo ni duni sisi tushiriki kujenga japo nyumba moja tu ya mwalimu ama daktari kweli wataona tupo pamoja nao.....
Ila tukibaki na hedikofta zetu na magari mapana yaliyoandikwa kub katu asilani kura zao tutazisikia redioni

ni kweli kabisa wapinzani hawajui kucheza na akili za maskini ambao ndo wananataka watu wa kuwasemea, wanakimbilia wasomi tu ambao pia hawakubaliki mbele za watu wasiosoma kutokana na kauli zao za kejeli
 
Haya ndio matatizo ya kudandia treni kwa mbele.

Na aliyekwambia mi nawadharau mafundi viatu ni nani!?
Au macho yako yana matatizo.

Mi nimesema kuwa mafundi viatu wengi mjini ni Wachaga!
Halafu we unakuja na maneno yako mabofu!
soma uelewe kijana sio kukurupuja tu!

mjomBA topic ya uzi huu inauliza hivi NI KWANINI CCM INAPENDWA MAHALI PASIPOKUWA NA MAENDELEO ? sasa badala ya kututoa kwenye MSTARI NI BORA UNGEJIBU HILO SWALI .
 
na mimi nashkuru kwa kudharauliwa na fundi viatu!

fundi viatu ni mtu mwenye ujuzi toka ulaya ,waafrika hatukua na ujuzi wa kushona viatu kabla ya mkoloni kuja. Mbona hatuwazungumzii wachaga malecturer,maengineer,madaktari,wahasibu,wanajeshi ,mafundi gereji, walimu,mapadri,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,wakulima n.k,,ninavyojua wachaga wako sekta zote almradi zinawapatia kipato,
 
ni kweli kabisa wapinzani hawajui kucheza na akili za maskini ambao ndo wananataka watu wa kuwasemea, wanakimbilia wasomi tu ambao pia hawakubaliki mbele za watu wasiosoma kutokana na kauli zao za kejeli

kumbuka kwamba lengo la hawa wapinzani ni kuwaokoa hao masikini na UHARAMIA WA SHETANI CCM , SASA UNAPOLETA MADAI YASIYO NA USHAHIDI UNATAKA KUMDANGANYA NANI NA KWA MANUFAA YA NANI ?
 
fundi viatu ni mtu mwenye ujuzi toka ulaya ,waafrika hatukua na ujuzi wa kushona viatu kabla ya mkoloni kuja. Mbona hatuwazungumzii wachaga malecturer,maengineer,madaktari,wahasibu,wanajeshi ,mafundi gereji, walimu,mapadri,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,wakulima n.k,,ninavyojua wachaga wako sekta zote almradi zinawapatia kipato,

Umewasahau mafisadi na matapeli wa kichaga pia!
Na wale wapika mbege mijini.
 
Hivi wachaga usipotutaja kwa siku huko nyuma kuna..te.kenya!?

Wacha kukataa kabila yako we mkerewe!
Unanuka vumba la samaki mpaka kwenye chupi yako halafu unajifanya mchanga!
Mtoto nuksi sana wewe.
Mfnsssssssss!
 
Na mimi nashkuru kwa kudharauliwa na fundi viatu!

Hivi wauza viatu wanaweza kuwa sawa na hawa wauza kahawa na kashata? wanaoshinda vibarazani wakipiga umbeya na kushindia mlo mmoja kwa siku? mimi ni msukuma lakini natambua maeneo yenye dhiki ni mikoa ya kanda ya kati,lindi,mtwara na pwani! nadhani huhitaji utafiti kubaini kuwa maeneo hayo yanakaliwa na watu wa aina ipi!!!???
 
There is an old saying which says " Education brings change in behavior……"

We kama unajiita msomi halafu bado unafuata mila chafu zinazoleta madhara ki afya! Basi hio elimu yako ni bure!
Huwezi kuita desturi zenye madhara ktk jamii (MILA)!

Na hii sio kusifia au kutukuza elimu za kizungu!
We mtu mzima ndani ya karne ya 21 bado unakunywa kinyesi cha mnyama kilicho changanywa na damu!!?
Duhh!
Mkuu inabidi ubadilike kabla ya kuja kuugua maradhi yasiojulikana.
Sina haja ya mabishano zaidi, nataka unieleze uliona wapi watu wakinywa kinyesi kilichochanganywa na damu? maana kwa kuishi kwangu uchagani sikuwahi kuona hilo likifanyika. Sasa nashangaa ulivyopigia mstari kiasi hicho. Kinachokusumbua nimeshakifahamu mkuu, si kingine bali ni chuki dhidi ya wachaga. Haipendezi hata kidogo mkuu, mi ningependa tufanye malumbano ya ana kwa ana ili nikuonyeshe jinsi ulivyokua na mawazo mgando.
 
Ndugu zangu naomba kuuliza ni kwanini maeneo mengi hasa vijijini wanaipenda sana ccm ilhali maeneo yanayowazunguka ni maskini wa kutupwa mliotembea mikoani nadhani hali halisi mnaijua yaani kuna maeneo kuanzia tuapate uhuru maji ya bomba hawajawahi kuyaona wala kuyanywa umeme ndio kabisaaa mbingu na ardhi ukienda kwenye huduma za afya ndio usiongee tukija kwenye elimu watu wanasomea chini ya mbuyu au kwa kifupi elimu sio lazima lakini hawa watu wanaipenda ccm balaa ni nini kinachowasukuma kuwa wakereketwa namna hii au ndio kutojitambua?
Unapotaka kuiponda biashara ya Nyama, ukiwa mjini inabidi uponde uchafu wa mabucha, poor health and safety issues zinazoonekana mfano nyama inadandiwa na nzi waziwazi, inapigwa na vumbi, muhudumu huna ukakika kama apron lake lililo tapakaa damu analifua on daily bases, nyama unapewa jamaa ajavaa hata glove mkononi ujui mikono imeshika nini tena kabla; yote hayo yanatishia ubora wa bidhaa na afya ya mlaji maana vijidudu nje-nje na kama ni nyama ya ndege salmonella hawakwepeki bila ya kusahau ulanguzi wa wenye mabucha. Tactic hiyo mijini itawafanya walaji wakusikie maana ni vitu ambavyo vipo wazi mbele ya macho yao.

Lakini ukienda kijijini na hadithi hizo hizo wengi watakuona mwehu (sio wote) kwasababu wengi wapo more concerned na kuuza n'gombe mzima kuliko alie buchani, wao wanataka kujua soko liko wapi aijalishi nyama ya mfugo inaenda ishia bucha ipi iwe na vumbi au supermarket ya kisasa cha muhimu mfugo uuzwe. Habari zako za uchafu wa mabucha na ulanguzi wa watu wa mjini zinaweza kuonekana zina mshiko upande wa afya hila mwisho wa siku si kitu ambacho kinamgusa mfugaji ambae anataka kuona mfugo umeuzwa hicho ndio kipato chake.

Ukirudi kwenye point wapinzani hawajui siasa za vijijini zinataka nini na zipo wapi kwa sasa, hivi wewe kila kijiji unachoenda unaongea habari za shule mbovu na wanafunzi kukaa chini, wakati serikari ndio kwanza ina angaika na wanavijiji wote kuwapeleka watoto shule kwa ulazima, kwa sasa wahusika wanasaidiana na taasi mbalimbali kuona watoto wanapelekwa shule na wanachukua nafasi zao za kuchaguliwa shule za sekondari.

Halafu wewe unaenda kuongea habari za shule mbovu ilihali hao wapiga kura (wazazi) wengi wao bado wanafundishwa umuhimu wa elimu na kuacha kuwapeleka watoto mashambani siku na wakati wa masomo, hapo sidhani kama tatizo ni wanakijiji bali wanasiasa ambao hawajaelewa ni nini hasa mwanakijiji kinamshawishi kupiga kura au anataka kusikia largely kwa sasa as an adult, that is to say tatizo sio watu wa vijijini it is the other way round tatizo ni uwezo na ufahamu wa viongozi wa siasa za upinzani na namna wanazotumia kuzungumza na wanakijiji kuna communication barrier regarding changes they are trying to sell.
 
Utafiti ulififanywa na wasomi wa chuo kikuu dar wamegudua chama tawala kinapendwa zaidi sehemu ambazo elimu ni duni na wanafunzi wanafeli mitiani, wakiongea na gazeti hili watafiti wa chuo kiuu dar wamesema hali hiyo inasababishwa na uoga na umasikini uliyokidhiri.vilevile watafiti wanasema kujitokeza kwa hali hiyo wakati mwingine inawafurahisha wana ccm na utawala wake
 
cheki pande za coastal hasa mtwara, lindi, rufiji, mkuranga, morogoro,tunduma, mahenge, chalinze, bagamoyo nk umaskini ni wa kutupwa lakini wao ccm nambari one tu!!!
 
cheki pande za coastal hasa mtwara, lindi, rufiji, mkuranga, morogoro,tunduma, mahenge, chalinze, bagamoyo nk umaskini ni wa kutupwa lakini wao ccm nambari one tu!!!

umasikini na ujinga ndiyo nguzo kuu ya ccm ! Na wanao mkakati wa kichama nchi nzima kuhakikisha wananchi wanakuwa masikini zaidi ILI WATOTO WAO WAENDELEE KUONGOZA MILELE ! WAMEANZIA KALENGA NA SASA CHALINZE .
 
mtaji wa ccm ni wanavijiji walionyimwa elimu yaani mafukara waliokata tamaa na maisha wasio kuwa na uhakika wa male kwa siku yaani wale mandina hao ndio mtaji wa ccm wakiingia na vipesa chai na andazi kwa vijana na chumvi kwa akina mama mbege akina baba lazima tuimbe ccm kwa njaa zote hizo kwa kikwetu tunasema owane nola ang'aye huo ndo mtaji wa ccm kutengeneza watu wawe mafukara wawatawale kama ilivyo chalinze na riz one
 
mtaji wa ccm ni wanavijiji walionyimwa elimu yaani mafukara waliokata tamaa na maisha wasio kuwa na uhakika wa male kwa siku yaani wale mandina hao ndio mtaji wa ccm wakiingia na vipesa chai na andazi kwa vijana na chumvi kwa akina mama mbege akina baba lazima tuimbe ccm kwa njaa zote hizo kwa kikwetu tunasema owane nola ang'aye huo ndo mtaji wa ccm kutengeneza watu wawe mafukara wawatawale kama ilivyo chalinze na riz one

jaPO UMECHANGANYANA KIKWENU LAKINI TUMEELEWA .
 
ni vizuri usiisome maana akili za kibavicha siku zote ni za kushikiwa. kwa kifupi wewe ni sawa na taburarasa. chadema ya wahafidhina inahitajika kuzimu, imependwa zaidi huko zaidi ya nyinyi mnavyoipenda. mungu wa kuzimu alitoa na sasa anatwaa. jina la huko kuzimu lihimidiwe. amen!

mwaka HUU LAZIMA CDM IKUTOE KIBYONGO !
 
Back
Top Bottom