1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
nadhani kati ya sababu ni mijadala kama hii inayoendelea, tunawatusi, tunawakejeli, tunawadharau, tunawashutumu, na hatutoi suluhisho kwao ...... Matusi yetu kwao, kejeli zetu kwao, dharau zetu kwao .....wao hutoa majibu kwenye sanduku la kura maana ndipo pekee wanapoweza kupaza sauti zao na kusikika...!
Vilevike nipendekeze jambo moja, ifike wakati tuache kuwadharau (japo pengine huonekana ni hali halisi) na kuonyesha tupo pamoja nao ktk shida zao ....tufanye kwa vitendo na si maneno matupu, .... Katika "say" wilaya ama tarafa nzima ambayo maendeleo ni duni sisi tushiriki kujenga japo nyumba moja tu ya mwalimu ama daktari kweli wataona tupo pamoja nao.....
Ila tukibaki na hedikofta zetu na magari mapana yaliyoandikwa kub katu asilani kura zao tutazisikia redioni
ni kweli kabisa wapinzani hawajui kucheza na akili za maskini ambao ndo wananataka watu wa kuwasemea, wanakimbilia wasomi tu ambao pia hawakubaliki mbele za watu wasiosoma kutokana na kauli zao za kejeli