Hivi kwanini jamii ya kitanzania hatuwezi kufanya biashara ya kifamilia

MZAZI ANAYE AMINI KUWA MALI KACHUMA YEYE NA MKEWE AU MUMEWE WATOTO WAKATAFUTE VYAO AWEZI KUJENGA UCHUMI WA HIVYO NDANI YA FAMILIA...UBINAFSI WA WAZAZI ...CHOYO YA WAZAZI ..MAFARAKANISHO YA WAZAZI NDIYO CHANZO...mzazi anaye amini kuwa watoto awapaswi kutegemea mali ya familia au urithi mzazi wa hivyo awezi kuifanya familia yake kuwa na uchumi wa pamoja.
 
Ni kweli pia japo nahisi watoto wetu wapo huru mno kujichagulia stadi za shughuli zao nje na zile zinazoweza kuubeba ukoo
 
Unampa fursa yeye anawaza ufe ili aone hapo unapotolea hizo fursa.
Yaaan acha kabisa mkuu

Nikikumbuka mzee wangu ndugu zake wamesema sio mtoto wa baba yao, ngachoka kabisa πŸ˜‚

Afu mtu anataka nikikutana nae nimsalimie, salamu yangu wataisikia

mpaka wanawaambia watu mtoto wa fulani hanisemeshi, mimi huyu kama hawamjui mzee wangu mm watanijua kama nani??

Mtu huwez mchukia mzazi wangu afu unipende mm ?

Mm nimetoka ndani ya maungo yake,

Eeh bana Mali zangu ni zangu hao mashangazi wakafie mbele!!!!
 
Wazazi wa hivyo ni wa kupigwa vita dunia imeshahama huko tupo kwenye kuwekeza hisa na miradi ya muda mrefu au estate sasa kijana ataanzaje from scratch wakati mzee umepambana na ukifa uendi navyo unaviacha unamuachia nani zaidi ya watoto wako? Kama ni ndio kwanini waanze upya kuliko kuendeleza ulipoishia
 
Hoja yako siyo sahihi kilogic ...hata kidini mungu anaweza kukupenda wewe asiwapende wazazi wako ...hivyo hoja siyo kuchukia au kuua au kupiga hoja hapo je wanamchukia kwa HAKI AU LA ...Tumia akili kama wanamchukia baba yako nao ndiyo walio mdhulumu au wanamchukia kinyume na haki ...basi tambua kuwa baba yako naye anawachukia sawa sawa na Haki ...ni kama katika nchi hata hapa Tanzania ...tunaye Rais muovu sana anaye wachukia Wazalendo na hivyo wazalendo nao wanamchukia huyo Rais muovu hivyo kunatokea kuchukiana ...hapo tunaona aina mbili za chuki
1)chuki dhidi ya haki na..
2)chuki kwa ajili ya haki
KWA HIYO WEWE KUSEMA NI LAZIMA ANAYE MCHUKIA MZAZI WAKO YEYE NDIYO MBAYA UNAKOSEA KWA SABABU JE IKIWA WANAMCHUKIA MZAZI WAKO KWA SABABU YEYE NDIYE MBAYA ?hivyo hapo unatakiwa KUHUKUMU KWA HAKI SIYO KWA KUTAZAMA MZAZI AU MJOMBA AU NDUGU AU MAMA NK ..TUONGOZWE NA HAKI SIYO UNDUGU URAFIKI , MAPENZI NK
 
Ni wazazi wasio na akili ...cha kushangaza utawakuta watoapo hoja za kusifia matajiri kama baresa ...sasa swali ukiwauliza je watoto wa baresa wanaanzia chini kabisa kutafuta maisha jibu linakuwa hapana maana wao uendeleza utajiri wa baba yao ndani ya familia hata kabla ajafa na wanaanzia kileleni kukuza uchumi ....sasa kituko ni wazazi wapumbavu wanao tamani watoto wao waanzie mavumbini kutafuta maisha
 
Hapo umezungumzia ishu za dini,

Ishu ni kusema baba yangu sio ndugu yao na hawajashare baba!!!

Na ni kitu serious nasemea,
Kama alikuwa baba yao na sio baba yake mzee

Iweje kipindi chote huyo baba yao ashinde na kuwa nasi Leo hii waseme sio baba yake ? Na wanafanya vikao vyao vya kishenzi !!

Mbaya zaidi wanawaambia watu wa karibu na sisi na bado utayasikia

Binafsi sina chuki na mtu maake sio ndugu zangu, ni ndugu wa mzee

Hata mmoja wa waliosema mzee sio ndugu yao alipass away lakini mzee alienda

Mimi sikuenda sehemu yoyote maake mtu sina mawasiliano nae 10+ yrs na upuuzi wao mwingi tuu

Mambo ya Mungu yaache kwanza, tudili face to face
 
Ujaelewa nilicho kusahihisha soma tena kwa kutumia akili ...
Chuki imegawanyika kwenye makundi mawili
1)haki dhidi ya batili
2)batili dhidi ya ubatili
Mimi nilicho sema ni dhana yako kuwa amchukiaye baba yako awezi kukupenda wewe ...nikakuambia kuwa siyo sahihi inategemea hiyo chuki ni ya namna gani ...mfano wewe unaweza kumchukia kaka yako tena kwa haki kabisa kutokana na ubaya aliokutendea ila usiwachukie watoto wake .....ila kwenye tukio ulilo sema wewe kuwa baba yako ndiyo walimtendea vibaya hao ndugu zake maana yake HAKI haipo upande wao ipo upande wenu hivyo ni sahih9 wewe kuwachukia na kuwaepuka .
Mfano wa mwisho usipo elewa basi ...mfano ingekuwa baba yako ana chukiwa na kaka zake kwa sababu huyo baba yako ndiye aliye wakana hao kaka zake ili apate mali nk na akafanya hivyo ...hivyo baba yako ndiye muovu kwa kaka zake ...maana yake kungekuwa na chuki pia baiba ya baba yako na kaka zake ila ni kinyume na ilivyo sasa ....je wangekupenda wewe licha ya baba yako kuwa ndiye aliye watendea ubaya unge chukia ?
 
Haiwezkn nina akili timamu wakwende wakafie mbele..... Kila mtu na mambo yake
 
Aiseee. Kazi unayo. Hahaahaa.
 
Biashara kubwa (umetaja Bill Gates) haziendeshwi kifamilia.
Ni public listed company inayouza hisa zake kwenye soko la hisa(alama ya hisa: MSFT kwenye NASDAQ) na ina mamilioni ya wawekezaji duniani kote.Kwa sasa, Bill Gates haishughulikii tena Microsoft moja kwa moja na anamiliki asilimia ndogo tu ya kampuni.Uamuzi wa kampuni unafanywa na wakurugenzi na wasimamizi walioteuliwa kitaaluma, si wana familia.
 
mzazi anahofu ya kutolewa kafara muda wowote πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜
 
Ukae pamoja na ukoo wa kibongo, wakuroge? No thanks πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Bora biashara umrithishe mwanao tu, hao mashangazi wasubiri kwanza
 
Yes! Wataalamu wa masuala ya fedha ndio wasimamizi lakini wamiliki wa share/hisa ni wanafamilia na sio individual
 
Ukae pamoja na ukoo wa kibongo, wakuroge? No thanks πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Bora biashara umrithishe mwanao tu, hao mashangazi wasubiri kwanza
Watoto wenyewe pia tunazaa mseto kurogana kupo palepale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…