Hivi kwanini jamii ya kitanzania hatuwezi kufanya biashara ya kifamilia

Kwa maoni yangu, pamoja na sababu zingine, idadi ya watoto kuwa wengi inachangia pia
Mfano, kwa mali kidogo iliyopo na mzee ana watoto say 7, ni ngumu kuwatosha au kuwashirikisha wote, hapo ndipo kauli ya tafuteni mali zenu hujitokeza

Ila kama mtoto ni mmoja au wawili ni rahisi kuwafundisha na kuwarithisha
 
Hadi naandika uzi ujue kishanilamba
Pole sana Money and Blood don't mix Mkuu. Ili mfanye hiyo biashara ni lazima kuwe na mfumo imara wa nidhamu kwa wote na iwepo kwenye mfumo wa kisheria.

Zipo biashara za kifamilia za ndugu waafrika hapa bongo na zinafanya vizuri tu pia.
 
Kwa sababu mna roho mbaya, husda, wizi, utapeli na mnaamini sana ushirikina.

Hamuamiani kabisa, hata mwanao anakuibia na mke ndio usiseme kabisa

Tofauti na jamii zingine ambazo zinaamini kuacha kitu kwa vizazi vyao
Alafu kwenye familia mmoja
Anajifanya mjuaji,kila kitu kaachiwa yeye
Refer,kuuza mali(nyumba)familia

Ova
 
Kwa sababu mna roho mbaya, husda, wizi, utapeli na mnaamini sana ushirikina.

Hamuamiani kabisa, hata mwanao anakuibia na mke ndio usiseme kabisa

Tofauti na jamii zingine ambazo zinaamini kuacha kitu kwa vizazi vyao
Unakuta tu watoto wako 4
Wanaachiwa nyumba potential area unakuta kaka l/dada anajifanya mjuaji anatumia ukubwa wake kuwakandamiza wenzake kama kodi anakula pekee yake mwisho wa siku
Wenzake wanaamua pauzwe kila mtu afe na chake

Ova
 
Mfano mzee kaacha nyumba moja center ambayo Ina fremu za kupangisha kama kumi na nyingine ya kuishi pamoja na shamba. Watoto akawa nao 15

Kwa idadi hiyo hao watoto wanashindwa vipi kuweka Mali za mzee wao kwenye uangalizi na wakazisajili na kuziendeleza, wakapangisha fremu zote na mashamba (kama hamlimi) mkaanza kukusanya mitaji na kuwekeza zaidi huku mkiendelea kupeana gawio yani mnaishi kama alivyokuwa anaishi mwenye Mali

NB, hii inawezekana kama wote 15 mtaamua kujishughulisha na mambo mengine zaidi ya kutegemea mali ya baba pekeake kwani wengi kati yenu 15 mtakuwa niwatu wazima mnaojitegemea

Huu ni mfano tu
 
Pole sana Money and Blood don't mix Mkuu. Ili mfanye hiyo biashara ni lazima kuwe na mfumo imara wa nidhamu kwa wote na iwepo kwenye mfumo wa kisheria.

Zipo biashara za kifamilia za ndugu waafrika hapa bongo na zinafanya vizuri tu pia.
Tofauti na familia ya Mengi kuna zingine
 
I dont think so. Mimi nimefanya kazi na wahindi na nimejaribu sana kuchanguza maisha yao. Namba moja ni kuwa hawajaathirika kama sisi na utamaduni wa kimagharibi. I mean bado kwenye familia zao wanaishi yale maisha ya kufuata misingi ya jadi i.e. mkubwa ndiyo kinara na anaheshimika kweli kweli. Labda jambo la kuzingatia ni kuwa hata hao wakubwa wanaoheshimiwa nao wanajiheshimu na wana nidhamu ya kazi. Mwafrika 1. hana nidhamu ya kazi na anatosheka mapema sana. 2. Anapenda anasa hasa wanawake. 3. Ni mwizi na anapenda ujanja ujanja.
Ndiyo maana nikakukatalia kuwa tatizo siyo kushirikisha watoto kwa sababu watoto wengin wanapopewa nafasi ya kushirikiana na wazazi au jamaa zao huiba na kukimbilia starehe bila kusahau short cut ya kutaka mafanikio.
 
Kwani hawajatoboa?
Mada inazungumzia mali kutokugawanywa kwa warithi!!

Mali za marehemu Mengi ni LAZIMA zitagawanywa kwenye hiyo kesi yao ya mirathi.

Means hawatatoboa kuwa miongoni mwa familia ambazo mali haikugawanywa kwa warithi.
 
Mwafika sijui ni nini anachoweza. Akipata kidogo matako hulia mbwata. Angalia watu kama kina Lugumi. Lugumi angekuwa ni mhindi wala usingejua kuna mtu kama huyu kwa sababu ange-operate chini chini kuongeza utajiri wake. Lakini kwa mwafrika anaona keshamaliza kila kitu kiasi cha kutembea na msafara na kujigamba kila sehemu,
 
Unakuta tu watoto wako 4
Wanaachiwa nyumba potential area unakuta kaka l/dada anajifanya mjuaji anatumia ukubwa wake kuwakandamiza wenzake kama kodi anakula pekee yake mwisho wa siku
Wenzake wanaamua pauzwe kila mtu afe na chake

Ova
Yaani kuna mambo unajiuliza na kujibu kuwa umasikini mwingi unasababishwa na ubinafsi na roho mbaya.

Nimeshuhudia vijana wamemuuwa baba yao ili wagawane mifugo.
Baba kafa wamegawana mifugo yote zaidi ya elfu moja
Baada ya miaka mitatu hata mazizi hayajulikani tena.

Wamemuacha mama yao mjane bila sababu za maana.

Unakuta wengi wana akili za hivyo.
Mtu anapewa fursa ya kujiendeleza Badala yake anakulia timing akumalize

Unadhani watakuja kuwa na kampuni watu kama hao
 
Ulichokiandika hapa,ndicho nilichokiandika mimi kwenye last paragraph ya comment yangu uliyoiquote,
Comment yangu ina zaidi ya hoja moja,kanisome tena.
 
Mtu anayemuua Baba yake ili arithi hiyo mali,hawezi kuendelea coz hana akili,mtu mwenye akili timamu hawezi kumuua Baba yake kisa mali,

Hao walisha feli baada ya kumuua Baba yao,pia mali ya dhuluma hua haina baraka,hupukutika na kupotea na itakutesa sana mpaka umauti utakapo kufika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…