Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Ukweli hii ni aibu. Zama hizi si za kuzuiwa kusafiri eti kisa tunawaogopa majambazi wahuni kutoka burundi na rwanda. Nchi yetu ina majeshi imara why tusiyatumie? Kama mmeshindwa kabisa tuingie mkataba tu mi nna mercenaries solders waliokuwa well trained kuwa disessminate hao wavuta bangi wote within no time.
 
Mkuu ni kwa usalama wako ,Kuna story ya Jambazi Mtoto Jonathan Meshack aliyetikisa kanda ya ziwa miaka ya 2003-2012 ,alipiga matukio ya hatari ya utekaji kwenye mapori ya nyakanazi na mengine mengi tu na kukwara mali za basi zima.

Hizo sehemu ni hatari kukatiza especially usiku...Kama una haraka sana ni bora uwe unapanda NDEGE au tumia private car upite mida unayotaka wewe peke yako.
 
Hawataki kusema tu, uwa wanafanya hivi kuwapisha wachawi kufanya yao usiku
 
Panda ndege mkuu,
 
wewe naye hiyo ni route gani dar-mpanda apite tena kaliua?
 
Hii mambo magufuri ailiikataa enzi zake.
 
Hahaha Mkuu
Na chimbo langu hapo ...nikitoka Arusha na Coast line lazima nipige chini...napokelewa na Dubai ya Sikonge ..overnight 3 days!!!!
 
Ushawai kusikia bus kutekwa na majambazi au ww ulikua bado kwenye mbupu.
Miaka ya 80 kweusi habari hizo zilikuwepo sana kwenye hayo mapori.
Nilishuhudia kuna siku hapo kati Manyoni ukitoka saranda ukaanza kuitafuta manyoni shughuli pevu.
Kilimatinde lilipigwa tukio,tulikuta wazalendo wameweka gogo barabarani.
Bado kusimama walume wakaibuka toka porini nyuma na mbele.
Kuna mwenye jegeje mkanda anao full una njegere za kutosha
Akatwanga juu km 20 hivi kwanza.
Kisha mnaambiwa teremka vua kila kitu acha pale kalale pale chini.
Jamaa walikomba kila kitu cha abiria hadi maandazi na maharage enzi hizo chipsi mayai haijazinduliwa.
Wakachukua mizigo yao wakazama msituni.
Fikiria mnaachwa bus zima uchi.
Hamna cha baba,bibi,babu ,mtoto uchi wa mnyama.
Mnarudi kwenye Bus kuendelea na safari na umbea wetu wabongo ndio mnachunguzana sasa huyu kumbe govinda'huyu kumbe kakeketwa huyu ana mbunye kubwa hivi.
Mpk Bus inafika polisi dereva akapiga ukunga akiwa uchi pia ndio kuja afande kupewa ripoti.
Zikatafutwa kanga mradi watu wajisitiri.
Sasa ww ukikatazwa kwenda mda huo polisi washajua kuna wababe wao hapo kati.
Ina maana bora lawama hizi unazotoa kuliko muende mpigwe tukio huko kati badae mtalaumu kwanini hawakuwazuia.
 
Hivi huko kwenye hayo mapori, hakuna namna serikali inaweza kufanya jambo, kama kuweka vituo vya ulinzi kwa ajili ya wanajeshi/askari ili kuleta usalama?

Kwasababu kitendo cha kuzuia abiria kusafiri usiku, ni sawa na kukubali kuishi na majambazi ndani ya nchi yetu, hili naona halistahili kuwepo.
 
Aisee ...
 
Babu nimecheka kama mazuri vile.
 
Hahaha Mkuu
Na chimbo langu hapo ...nikitoka Arusha na Coast line lazima nipige chini...napokelewa na Dubai ya Sikonge ..overnight 3 days!!!!
Mkuu hata mimi ndio njia yangu kwenda Swanga, Wewe umesema ukweli kinachoendelea. Naona mapoyoyo yanabishana kwamba hiyo barabara ina utekaji. Ukiwauliza ni lini Utekaji umetokea mara ya mwisho hawana majibu🤣🤣. Magufuli alipoingia mwaka 2015 akawaambia maRPC hataki kuskia utekaji na pia askari asipande basi kuescot hicho kitu njia hiyo hakijawahi tokea hata kabla ya hapo nadhan tokea 2013 yaani miaka 10 iliyopita hakuna tukio.
Sasa Magu kaondoka tumerudi zama za Mawe kuogopa Majambazi ndani ya Nchi huru.
Madereva wakatumia hiyo loophole wakaweka Vimada Sikonge sasa imekua kero kero kero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…