Hivi kwanini mnapenda Biriani? Sijawahi kupenda Biriani

Hivi kwanini mnapenda Biriani? Sijawahi kupenda Biriani

Huwa wanakula biriani za vichochoroni hao 😀😀😀
Biriani huwa linapikwa mpaka ile nyama inakuwa laini kushinda mkate wa Super loaf 😀😀😀
🤣🤣🤣Kwa hiyo mi nimekula la vichochoroni?Umeanza lini dharau we mtoto?
 
Kiukweli kabisa mimi pia najiona mshamba,bora nile wali maharage kuliko hiyo biriani.

Pale nyama tu naweza sema napenda.
 
Mie nyumbani ndio mpishi yani mkewangu hapikagi hupika mara mbili tu kwa wiki.
Pishi gani la mchele unataka kulijua!?
-Wali wa dikodiko.
-Biryani.
-Mandhi.
-Bokoboko.
Pilau na wali wa kawaida najua ni jepesi.
Mandhi pleaseeeee....
 
Ni upuuzi tu wa wabongo kupenda kwenda na upepo, kitu cha kijiiinga ila kinaweza vumishwa utasema ni nini sijui.

Birian nilipokua nasikia sikia nikajua ni kitju flan amazing sana. Halaf stupid enough, ikawa utamaduni kwamba mahala pengi maarufu birian inapikwa IJUMAA tu!. Siku nikasema acha nikatoe ushamba, aaaahhh nikakuta ujinga uuinga kabisaa.

Ni tamu birian ila sio kwa sifa na umashuhuri inayopewa.

Same same applies ni kitu flan kilivuma sana hapo nyuma , MAKANGE.
Makangeee makange, siku niko around maeneo ya Masaki , nikasema acha nisogee Jackis pale , nikaagiza makange ya kuku, doooohhhh!! I was very suprised, ni kuku tu wa kawaida sema minyanyaa na miviungoo ndio imesheheni. Ujinga kabisaa.

Ikaja ujinga mwingine maarufu wa vyakula kwa jina la KISINIA.

Yan wabongo wanapenda sana ku "trend-sha" vitu sana
Kweli kabisaa,makange nayo mmmmh yalitutesa kabla hatujayajua😁
 

Attachments

  • 20230804_134453.jpg
    20230804_134453.jpg
    897.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom