Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Yaani Urusi imevunja makubaliano yaliyofanywa baina yake, NATO na Ukraine kuhusu silaha za nyuklia. Kuna jamaa mmoja aliandioka kuwa hilo ni kosa kwa vile Urusi itaweza kuinyanasa Ukraine, ila Ukraine wao waliamini kuishi bila uadui, sasa hivi putin amewaharabia nchi yao kwa kubomoa karibu kila kitu na kuuwa watu hovyo. Halafu eti anataka Ukarine iandike kuwa haitajiunga na NATO ilhali yeye tayari alishaonyesha kuwa haheshimu makubalino. Kinachonisikitisha ni pale NATO imeshindwa kuingilia kati kuiokoa Ukraine na uharibifu huo.Ukraine waliambiwa msiwe na nuclear mkiingiliwa Kivita tutawasaidia. Matokeo yake tumeyaona. Sasa inavyoonekana kichaa Putin ataanzisha www 3 maana haambiliki Sasa Hivi. Sasa Sisi nchi za Africa tutatetewa na NATO au ndio basi.
Kitu kimoja nimejifunza, ni kuwa jeshi la Urusi ni dhaifu sana, ila lina mabomu mengi na makombora mengi ambayo ndiyo wanatumia tu. Inapokuwa kupambana ana kwa ana wamekuwa wanashindwa vibaya sana. Wanategemea mabomu ndiyo yafanya kazi ye kuua watu karibu wote kwenye mji halafu wao waingie kukiwa hakuna upinzani wowote.