Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

[emoji3059][emoji3059][emoji3059]
Screenshot_20201113-110912_Gallery.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Hivi kwa nini Tanga ni Jiji, maana naona pilikapilika kama za majiji mengine hazipo kabisa, ni Mji ambao umepoa mithiri ya Tabora, baiskeli huku ndio nyingi kuliko magari.

Vijiwe vya vijana vipo kila mahala, huku maisha ni mepesi sana, yaani ukiwa na 500 unakula ugali na mboga za majani.

Ukienda kula wali samaki unapewa kibua mzima na wali eti elfu 2. Nyumba za majani zipo mpaka katikati ya mji, nyumba zenye vibaraza vikubwa zile za kizamani ndio zimejaa.

Nyumba za matofali ya tope zipo kila mahala. Nyumba za miti pia bado zipo.

Wale wanawake wazuri wa Kitanga wala huku siwaoni kabisa, hivi hii ndio Tanga niliyokuwa naisikia nikiwa Dar es Salaam. Au kuna Tanga nyingine wakuu? Tofauti na hii ya Forodhani, Chumbageni, 16, Donge, Majani Mapana, Gofu Chini n.k.

Sehemu za kula bata Tanga hazipo kabisa. Wanawake wa huku wanapenda wageni sana kuliko wenyeji sijui kwa nini?

Kiukweli Tanga ni sawa na Tabora tu, Wala Tanga haina hadhi ya kuwa Jiji.
Tanga sio jiji na halijawahi kuwa jiji acha kukurupuka fanya uchunguzi
 
Tanga sio jiji na halijawahi kuwa jiji fanya uchunguzi usikurupukie mambo
Mji wowote wenye Bandari zaidi ya moja kama Tanga,automatic ni City(,jiji,).
1.BANDARI KUU YA MIZIGO,KATIKA BAHARI YA HINDI ,IKO TANGA.
2.BANDARI ZA KUPOKEA MAFUTA,TATU TOFAUTI.
3.BANDARI YA KUSAFIRISHA ABIRIA.
4.BANDARI YA KUSAFIRISHA MAFUTA KWENDA,DUNIANI KOTE,BANDARI HII HAKUNA DUNIANI KOTE,NI YA AINA YAKE IKIWA IKO TANGA.BANDARI YA KUSAFIRISHS MAFUTA HUKU YAKIWA KWENYE MKANDAMIZO WA JOTO.
 
Mji Wenye Bandari,zaidi ya tatu,bandari za bahari kuu,inayounganisha majiji ya dunia,automatic mji huo,ni jiji.
 
Mji wowte wenye bandari,zaidi ya tatu,kupitia bahari kuu,kama Tanga,ikiwa bandari zaidi ya tatu,automatic ni jiji.Bandari hizo,huunganisha na majiji kadhaa ulimwenguni.Indian ocean city.
 
Back
Top Bottom