luangalila
JF-Expert Member
- Jan 12, 2014
- 6,375
- 6,986
Embu tuqmbie kwann unalalamikia nyumba za wananchi wenzako ?Hivi kwa nini Tanga ni Jiji, maana naona pilikapilika kama za majiji mengine hazipo kabisa, ni Mji ambao umepoa mithiri ya Tabora, baiskeli huku ndio nyingi kuliko magari.
Vijiwe vya vijana vipo kila mahala, huku maisha ni mepesi sana, yaani ukiwa na 500 unakula ugali na mboga za majani.
Ukienda kula wali samaki unapewa kibua mzima na wali eti elfu 2. Nyumba za majani zipo mpaka katikati ya mji, nyumba zenye vibaraza vikubwa zile za kizamani ndio zimejaa.
Nyumba za matofali ya tope zipo kila mahala. Nyumba za miti pia bado zipo.
Wale wanawake wazuri wa Kitanga wala huku siwaoni kabisa, hivi hii ndio Tanga niliyokuwa embu naisikia nikiwa Dar es Salaam. Au kuna Tanga nyingine wakuu? Tofauti na hii ya Forodhani, Chumbageni, 16, Donge, Majani Mapana, Gofu Chini n.k.
Sehemu za kula bata Tanga hazipo kabisa. Wanawake wa huku wanapenda wageni sana kuliko wenyeji sijui kwa nini?
Kiukweli Tanga ni sawa na Tabora tu, Wala Tanga haina hadhi ya kuwa Jiji.
Unalalamikia uwepo wa nyumba za viaraza virefu hujui kama TNG ni mjinwa historia huo ?
Isitoshe serikal ina vigezo vya kutoa hadhi ya mji kuwa jiji ..sasa yakupasa ufahamu kwann Tng ni JIJI
Lastly, unalalamikia nyumba za wenzako, mara bei ya msosi ipo cheap, ww umechukua hatua gani ya kubadilisha TnG hasa kwa hili la nyumba embu tuonyeshe nyumba yako ambayo ww umejenga hapo Tng