Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

Hivi kwanini Tanga hainyang'anywi hadhi ya kuwa Jiji? Ni sehemu ya ajabu sana

Ila kweli tanga duuuu....
Sijui kumbe adi wadada wazuri wakiwa wengi maali iyo sehemu ina hadhi yakuitwa jiji[emoji849]
Nafikiri hili ndio haswa lililompeleka huko.
 
Nafikiri yote uliyotaja kasoro yanayohusu ngono, ndio yaliyopelekea likawa Jiji. Kama wewe huoni basi ni udhaifu wako.
Mkuu vipi majani mapana, mapinduzi,nguvumali, donge,Gofu chini/juu, Airport.

Kuna sehemu moja hivi wanapaita uzunguni huko ndio kuna vyumba self za 70/80. Yaani huko ndio wanaishi wenye unafuu wa maishaa Tanga. Sehemu ambapo hata Mbezi ya Kimara inamajengo mazuri kuliko Uzunguni Tanga.

Nyumba unapata kwa bei ya 180,000 ya vyumba vinne, kimoja master.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Acha kufananisha mboka na vitu vya kipimbi
 
Tanga ilianza kuendelea kabla ya Arusha na Dar, Hata vitu vingi vimeanzia tanga nikukumbushe tu Hydro Power station ya kwanza ilikuwa Tanga Hale MW 21 na ilizinduliwa na Baba Wa Taifa Nyerere 1964, Shule ya kwanza ya serikali ilijengwa Tanga nayo ni Tanga technical school Aliposoma Rais mstaafu Kikwete, Tukisema Viwanda Tanga ilitisha sana
 
Tanga ya maajabu sana! Angalia
1. Mtoto atapigwa afe kama hakwenda "chuo", lakini formal school ni hiari yake!
2. Mwanamke anajipamba malaki mwilini lkn angalia nyumba anakotokea, hata Mbwa hawezi kukaa
3. Ni rahisi kuvunja ndoa kuliko kukosa dera.
4. Mwanamke kuwa na Madera 50 ni kawaida
5. Harusi ya kufa MTU ni kibarazani kwenye hema moja, " kinywaji" ni maandazi, maharage , ugali na muziki wa nguvu kwa siku tatu
5. Dini ya mtume SAW ni maisha yao Alfa na omega
6. Mzazi kumtukana mtoto matusi ya nguoni makali mfn mb....ya baba yako kawaida sana mbele ya kadamnasi.. udigoni

7. Mahari ni maelewano kati ya binti na kijana. mara nyingi huwa binti anataka godoro na ni lake akiachika analibeba

8. Ongezea......
 
Mkuu vipi majani mapana, mapinduzi,nguvumali, donge,Gofu chini/juu, Airport . Kunasehem moja hivi wanapaita uzunguni huko ndio kuna vyumba self za 70/80., Yaani huko ndio wanaishi wenye unafuu wa maishaa Tanga. Sehemu ambapo hata Mbezi ya Kimara inamajengo mazuri kuliko Uzunguni Tanga.

Nyumba unapata kwa bei ya 180,000 ya vyumba vinne, kimoja master.
Uzunguni ndio wapi? Watu wenye Hela Tanga wanaishi
1. Raskazone
2. Sahare ya upande wa baharini
3. Mwambani

Raskazoni kuna nyumba kibao kodi ni zaidi dola 1000, sidhani kama kuna nyumba ya 180k kule hiyo ulioitaja.
 
Tanga ilianza kuendelea kabla ya Arusha na Dar, Hata vitu vingi vimeanzia tanga nikukumbushe tu Hydro Power station ya kwanza ilikuwa Tanga Hale MW 21 na ilizinduliwa na Baba Wa Taifa Nyerere 1964, Shule ya kwanza ya serikali ilijengwa Tanga nayo ni Tanga technical school Aliposoma Rais mstaafu Kikwete, Tukisema Viwanda Tanga ilitisha sana
Mpaka leo Tanga ina viwanda vingi, kuna asilimia kubwa mtoa mada maisha yake toka amezaliwa anategemea products za Tanga mpaka anakua.
 
Tanga ya maajabu sana! Angalia
1. Mtoto atapigwa afe kama hakwenda "chuo", lakini formal school ni hiari yake!
2. Mwanamke anajipamba malaki mwilini lkn angalia nyumba anakotokea, hata Mbwa hawezi kukaa
3. Ni rahisi kuvunja ndoa kuliko kukosa dera.
4. Mwanamke kuwa na Madera 50 ni kawaida
5. Harusi ya kufa MTU ni kibarazani kwenye hema moja, " kinywaji" ni maandazi, maharage , ugali na muziki wa nguvu kwa siku tatu
5. Dini ya mtume SAW ni maisha yao Alfa na omega
6. Mzazi kumtukana mtoto matusi ya nguoni makali mfn mb....ya baba yako kawaida sana mbele ya kadamnasi.. udigoni

7. Ongezea......
1. Unazungumzia mwaka gani huo..?
 
Tanga sijui kwanini hakuendelei kila nikienda pako vile vile
 
Nimesoma tanga A level kiukweli naipenda sanaa tanga,ni mji mtulivu sanaa kwa kuishi .naomba wenyeji wa huko wanijuze bei za viwanja maeneo ya kange ,makorora au usagara
 
Nimesoma tanga A level kiukweli naipenda sanaa tanga,ni mji mtulivu sanaa kwa kuishi .naomba wenyeji wa huko wanijuze bei za viwanja maeneo ya kange ,makorora au usagara
Makorora na usagara unamtoa Mtu, ngumu kupata viwanja, kange unapata. Kama ni Banda tu unaweza pata around 20m
 
Hivi kwa nini Tanga ni Jiji, maana naona pilikapilika kama za majiji mengine hazipo kabisa, ni Mji ambao umepoa mithiri ya Tabora, baiskeli huku ndio nyingi kuliko magari.

Vijiwe vya vijana vipo kila mahala, huku maisha ni mepesi sana, yaani ukiwa na 500 unakula ugali na mboga za majani.

Ukienda kula wali samaki unapewa kibua mzima na wali eti elfu 2.

Nyumba za majani zipo mpaka katikati ya mji, nyumba zenye vibaraza vikubwa zile za kizamani ndio zimejaa.

Nyumba za matofali ya tope zipo kila mahala. Nyumba za miti pia bado zipo.

Wale wanawake wazuri wa Kitanga wala huku siwaoni kabisa, hivi hii ndio Tanga niliyokuwa naisikia nikiwa Dar es Salaam.

Au kuna Tanga nyingine wakuu? Tofauti na hii ya Forodhani, Chumbageni, 16, Donge, Majani Mapana, Gofu Chini n.k.

Sehemu za kula bata Tanga hazipo kabisa. Wanawake wa huku wanapenda wageni sana kuliko wenyeji sijui kwa nini?

Kiukweli Tanga ni sawa na Tabora tu, Wala Tanga haina hadhi ya kuwa Jiji.
Sijui kwa nini ukilisema jiji La Tanga watu wambeya jiji nao wanamind!. 😁😁😁
 
A ha ha ha mkuu Tabora napaheshimu nimesoma form one mpaka form four Tabora, lkn haina utofauti na Tanga, baskel kila mahala.
Pamebadilika sana mkuu saiv mapikipiki kila kona 😅😅
 
Back
Top Bottom