Fashion Fashion Fashion
Sio kila mwanaume mrefu hupendeza akivaa suti,
Sio kila mwanaume mfupi huchukiza akivaa suti,
Kuna vitu vingi sana vinachangia mtu kuonekana kapendeza kuanzia
Rangi ya Ngozi yake
Umbo lake
Style ya Nguo aliyovaa
Rangi ya Nguo anayovaa
ingekua ufupi ni tatizo,basi hakuna mtoto ambae angekua anavalishwa anapendeza,na wote tunajua hakunaga mtoto mrefu otherwise uzae ROBOT.
Mtoa mada nipende tu kukwambia taste za wanaume unaowapata ni washamba na wasiojua fashion,japo "wana pesa" maana unaonekana unaangalia zaid wallet wewe,unasahau wallet haina uhusiano na Fashion.
sikia nikwambie hao size men wako hebu wambie waache nunua suti za dukani na waanze sasa kushona suti kulingana na maumbo na kimo chao,Suti haijawahi mchukiza yeyote anae ivaa.
ukiona mtu kachukiza akvaa suti ni either
kavaa Suti ya dukani sio size yake
kavaa Suti yenye kitambaa cha rangi ambayo haiendani na ngozi yake
kashonewa suti na fundi asiejua Suti inashonwa vipi na bega linafanyiwaje finishing
Suti ni vazi Adimu, Suti inampendeza JOTI wa orijino COMEDY halafu imchukize huyo mwanaume wako?
Suti inampendeza Kelvin Hart halafu unaisema nini wewe, kuna raia wafupi kama Joti na Kelvin Hart?
Ushawakuta wakiwa wametupia vyombo vyao kwenye ma red carpet? Sikia mkuu Acha date na vibabu wababu huvaa suti OLD FASHION na zinazonunuliwa madukani.
Anza ku date rasmi na vishotii vyenzako vyenye chada ambao wao suti wanashonesha,unavaa Suti halafu unaenda nunua suti Sandaland,utakua unaumwa akili, mtoa mada suti haina uhusiano na ufupi.