Hivi kwanini wanawake wengi wakiwa mabinti (19-24 years), wanachagua ku-date na wanaume wa hovyo?

Tamthilia za kiphilipino zimechangia kuharibu vijana na mabinti wengi wa 2000s. Wanapenda maisha ya kuigiza na kutaka show off kumbe uzuri wa muonekano ni jambo mda tu
 
Unasemaje kakutakaa wewe kamkubali mtu wa hovyo. Unajijuaje wewe sio wa hovyo kwake huyo dame?

Dogo, mbona simple tu. Ukiona unakataliwa jua wewe wa hovyo, na mbaya zaidi wewe ni wa hovyo kuliko huyo boda aliyekubaliwa
Afundishwe upya Johari window 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
We jamaa mwaka jana napo ulianzisha uzi kama huu.

KUna shida mahali
Uo ulikuwa ni WA binti flani wa mtaani kwetu, binti alinikataa, mtoto wake wa kwanza akaenda kumzalia mume wa mtu, kuna picha juzi nliziona mtandaoni ndo nkazileta tena huu uzi GenuineMan
 
Juzi nimeona kabinti mahala kanaonekana kadogo ivi kama hakajazaa. Nikaomba namba nikapewa, ile siku sikumtafuta. Kesho yake asubuhi ikakuta sms “mambo” nikaliunga. Katika mazungumzo lahaulaa kana watoto wawili. Nilichoka nikafuta na namba. Now days mabiti wanataka kuruka kwanza na watu wanaopenda kuruka sio waoaji. So vinaruka vikizalishwa vinaachwa
 
Mnawaonea! nyie mmezeeka ndio maana hamuwaelewi zama zenu zimepita
Ila vijana wenzao wanawaelewa teknolojia imebadilika.
Ni usemalo umri ndio unaotusumbua tunawaona wako tofauti na sisi. Ila wanachokisema watu hapa ni ile hali kuchagua na kudondokea pa ovyo ili hali kuna watu wa maana tu walimtaka
 
Nachokaga unakuta binti mdogo anazaa na mume wa mtu halafu anabattle na mwanamke mweny mume. Huwaga na jiuliza anajiamini nini.
 
Hata sisi wanaume tukiwa na umri huo 25 - 30 hua tunazuzuka na mabinti wenye matako makubwa, tunaacha wadada wazuri wife material. Baadae sana ndio tunakuja kuelewa kuwa matako hayasaidii chochote kwenye maisha, tunarudi kuoa wa kawaida.
 
HAKUNA MWANAMKE ANAPENDA NICE GUY,kama wewe ni nice guy badilika,mademu wanapenda watu wahuni huni.
Hao ni wale aged 17-23! Kuanzia 24 akili inaanza kufunguka kuwa kumbe ubishoo wa kulamba lips, milegezo na viduku haviwezi kulipa bills baada ya kuona wenzao wanaoolewa na aina ya watu wanaoolewa nao.
 
Kijana wa hovyo 😂 umeshindwa kujiongeza
 
Kwahio unashuri amuone Mwamposa kwanza? 😁
 
Hahahah
ulikuwa boya Pro Max
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…