Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

Biashara ya mawe ya matani mfano copper,mchanga wa chuma,nk hio mia ni ndogo utapata zaidi ya hio.
 
Yeah, kuna jamaa yangu miaka ya 2010 alikua anauza hadi milioni 500 kwa siku tena wilayani,, ila haikua faida, bali mapato ghafi
Kwa mapato ghafi sawa!!watu wanachanga kati ya mapato ghafi na faida ghafi
 
Zipo biashara nyingi sana zinazoweza kukuingizia kiasi hicho cha faida au hata zaidi. Fahamu tu kuwa biashara nyingi zenye mzunguko mkubwa faida yake huwa asilimia ndogo kwa hiyo zinahitaji mtaji mkubwa.

Fanya hivi, ili upate millioni 100 kwa siku kutoka riba za fixed account benki utahitaji uweke kiasi gani? Kima hicho cha uwekezaji kigawe mara tatu, jawabu lake ndio kiasi cha uwiano cha mtaji utakaohitaji kwa biashara itakayoingizia million 100 kwa siku.
 
Inaonekana waliochangia weng humu hawajui tofauti ya mauzo na faida.
Tuombe Mungu hii isiwe sample ya umbumbumbu wa kizazi hiki cha allucination!
Hiyo faida zungumzia kampuni za huduma[large tax payers] kama za mawasiliano au wazalishaji kama madini na si kwenye bazaar economy za kariakoo.
Labda kama tunajadiri biashara za sinaloa
 
Kupata faida (net profit ) ya million 100 kwa siku, hapo ni lazima mauzo yako yawe milioni 600 hadi bilioni moja kwa siku

So kuna muuza nguo/spare anauza wastani wa milioni 800 kila siku? Ukizingatia competition ya Kariakoo?

Kumbuka hapa tunazungumzia net profit sio, gross profit
Yaani ushatoa mishahara, kodi ya serikali, kodi ya pango na overhead nyingine
 
Mwenyewe nimeshangaa sana, mwingine anasema eti kwa saa, wastani wa milioni 100 kwa saa (net profit)

Yaani huyo mtu anatakiwa awe anauza milioni 800 hadi bilioni ndani ya hilo lisaa ndio abakiwe na net profit ya million 100
 
Kwa Abood inawezekana ila sio kwa siku, ni kampuni kubwa, hata makampuni kama Vodacom, ila sio maduka ya Kariakoo uingize wastani wa FAIDA ya milioni 100 kwa siku
 
Nendeni kwa mama wenga pale buguruni..uone Semi ngapi zinazopakia nondo,bati na cement kila siku kupeleka huko mikoani.

Watu kama kina Mo na Bakhresa hiyo pesa ni ndogo kuingiza kwa siku.

Waingizaji wa mbolea nchini na bidhaa mbalimbali za pembejeonnao wanakunja mkwanja mrefu sana .
 
Sahihi kabisa mkuu, Ndo mana nikamwambia KWA hilo BADO haliniingii akilini.
 
Ukiwa na chini ya hyo vipi mkuu
 
Kwa hiyo hapo huo mchakato wote kufanya kwa siku moja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…