Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

kiongozi million 100 ndogo sana kwa wafanya biashara watu wanaingiza milioni 500 kwa siku ijekuwa iyo 100.
Kwa biashara gani hiyo mkuu ebu weka na mfano basi tujue maana kariakoo hakuna biashara ya faida ya mil20 kwa siku
 
Acha uongo wewe. Unaijua milioni 100 au unaisikia tu? Halafu unaijua milioni 100 kama faida? Kungekuwa na mabilionea wengi sana hapa Tanzania. Ina maana kwa mwaka faida ni bilioni 29 kitu ambacho hata makampuni makubwa ni ngumu sana kufikisha. Faida kwenye Jeans moja kwa bei ya jumla inachezea Tsh 2000 hadi 3000. Sasa jiulize auze jeans ngapi hadi hiyo 3000 iwe milioni 100 kwa siku.
Watu wengine hata reasoning kidogo tu hawana watu wamewekeza kwenye uchimbaji madini lakini hiyo mil100 anaingiza ndani ya mwez na sometimes inafeli na niuwekezaji mkubwa. Sasa kariakoo kunauwekezaji gani hapo wa kuingiza mil100
 
Nendeni kwa mama wenga pale buguruni..uone Semi ngapi zinazopakia nondo,bati na cement kila siku kupeleka huko mikoani.

Watu kama kina Mo na Bakhresa hiyo pesa ni ndogo kuingiza kwa siku.

Waingizaji wa mbolea nchini na bidhaa mbalimbali za pembejeonnao wanakunja mkwanja mrefu sana .
Hujui biashara kijana wewe so unajua faida iliyopo kwenye semi ya nondo wew..tufautisha mauzo na faida...hakuna kitu kinachoitwa faida ya siku. Mwenzio faida anaihesabu pale mzigo unapoisha anatoa import taxes ambazo ni kama pasu kwa pasu na faida bado gharama za uendeshaji wa biashara na mishahara. Kinachobaki sio haba kwa kapuku kama wewe ila ni kilio kwa tajiri. Biashara haiko kama unavyodhani na usione semi zinapakia mizigo mingi hapo hailipiwi cash ni mwendo wa mali kauli sasa unapozungumzia faida ya mil100 kwa siku nakuona kichaa. Hizo ni faida za viwanda.
 
Zipo biashara nyingi sana zinazoweza kukuingizia kiasi hicho cha faida au hata zaidi. Fahamu tu kuwa biashara nyingi zenye mzunguko mkubwa faida yake huwa asilimia ndogo kwa hiyo zinahitaji mtaji mkubwa.

Fanya hivi, ili upate millioni 100 kwa siku kutoka riba za fixed account benki utahitaji uweke kiasi gani? Kima hicho cha uwekezaji kigawe mara tatu, jawabu lake ndio kiasi cha uwiano cha mtaji utakaohitaji kwa biashara itakayoingizia million 100 kwa siku.
Hapa inshu sio mtaji mkubwa,kwani kwa biashara yenye kuleta faida ya milioni 100 kwa siku lazima uwe mkubwa sana!!inshu ni MAUZO hapa ambayo yatakuletea faida hiyo,unaweza kuwa na mtaji mkubwa(stock) lakini mauzo yakawa madogo!!hebu niambie kwa biashara za kariakoo yupi anaweza kuwa na mauzo ya milioni 800-bilioni moja kwa siku?!!ndii aweze kupata faida hiyo??hata kwa wanaouza mitambo kama ya ujenzi wa barabara hawezi kuwa anauza kila siku!!kwani hao ndio unakuta akiuza item moja tu milioni 2!!
 
Wachana na Biashara za Kariakoo, fanya biashara ya mazao makavu.

Utazungusha hata billion 5 kwa siku bila shaka yoyote ile.
 
Nina rafiki yangu alikuwa anafanya kazi Aboud bus service,alisema hivi

Walikuwa na mabasi 20 yote yalikuwa yanafanya rout za dar Moro kila siku na basi moja hufanya rout tatu kwa siku kabla ya torch kuanza.

Mabasi mengi yanalipa au kuingiza fedha nyingi kupitia mizigo wanayobeba kwenye buti,hats Kama basi likiondoka bila ya abiria lakini wao hasara hawapati.Hivyo kwa pesa uliyoizungumza watu wanaingiza kwa siku mpaka wiki

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Biashara ya mizigo ni nzuri
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wapo wale wamama wanatokea iringa wakinga kama sijakosea tunashinda nao kariakoo kiukweli wanauza sana lakini si KWA M100 KWA masaa tena nguo, mkuu spare ni biashara nzuri sana na KWA faida uliyotaja naweza kukubaliana nawe ILA japo mtaji nao unabid uwe mkubwa mkubwa, ILA hili la nguo [emoji23][emoji23][emoji23] BADO nalitafakari
Biashara ya spare upate eneo zuri
 
Nendeni kwa mama wenga pale buguruni..uone Semi ngapi zinazopakia nondo,bati na cement kila siku kupeleka huko mikoani.

Watu kama kina Mo na Bakhresa hiyo pesa ni ndogo kuingiza kwa siku.

Waingizaji wa mbolea nchini na bidhaa mbalimbali za pembejeonnao wanakunja mkwanja mrefu sana .
Biashara ya pembejeo inalipa Sana aiseee
 
Kumbuka huwezi kuingiza faida ya milioni 100 kwa muda ulosema kwa mtaji wa milioni mia mbili au hata milioni mia tatu au nne. Kwanza capital, pili aina ya biashara, tatu idadi ya wateja iwe large scale.
Nimeshuhudia kuna watu wanaingiza faida milioni mia tano kwa siku pale Kariakoo. Biashara ya simu za jumla wale ma agent waloingia ubia na viwanda vya simu China. Unakuta wafanyabiashara wote wanachukua mzigo kwake na kila Pisi moja unakuta faida elfu 5 tu na viswaswadu unakuta faida hadi buku tu. Sasa kwa siku anauza katoni nyingi sana za smartphone na viswaswadu brands zote itel, tecno, infinix, samsung n.k Na katoni moja mara nyingi ina simu 60pcs au 40pcs.
 
Nendeni kwa mama wenga pale buguruni..uone Semi ngapi zinazopakia nondo,bati na cement kila siku kupeleka huko mikoani.

Watu kama kina Mo na Bakhresa hiyo pesa ni ndogo kuingiza kwa siku.

Waingizaji wa mbolea nchini na bidhaa mbalimbali za pembejeonnao wanakunja mkwanja mrefu sana .
Umeambiwa kariakoo wewe

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom