Hivi kweli kuna biashara ya kuingiza faida kuanzia milioni 100 na kuendelea kwa siku/wiki/mwezi?

Wakati unashuhudia wewe ulikuwa kama nani hapo mbona mnaleta visasili wakuu? Unaijua FAIDA YA MILIONI 100 KWA SIKU? . Huyu mtu kaingiza kiasi Gani siku hiyo mpaka atoe makorokoro yooote kuanzia mtaji,malipo Kwa wafanyakazi nk. Alaf mkononi mwake ibake MILIONI 100 kama FAIDA
 
Halafu inakuwaje watu wanakuja kufirisika? Kuna jamaa yangu hapa SHY alikuwa akikaribia kufunga ofisi sasa apeleke pesa benki anajaza sandarusi kwa kukanyaga na miguu! Leo hii eti yuko kwenye mawe! Inasababishwa na nini?

Mbinu ya kuzilinda zibaki kuwepo huwa ni ileile uliuoyumia kuzipata, alishindwa.
 
Bora wewe mkuu umeongelea ngazi ya kiwanda sio kiduka wala kistoo kariakoo
 
Silent anaweza ingiza kupitia loose cargo ila hapati faida hiyo kwa siku.
Kwa wiki yawezekana kabisa.

Kina MO, Azam wanaingiza hiyo faida kwa siku
Dar ina watu takribani milion 8 na Bakheresa anamudu kuwauzia watu milion pekee jijini Dar zile Energy zake tu.

Fanya hesabu kila pieces mona apate faida ya 150 tu. Math 150×1,000,000/=150,000,000/= anapata faida kwenye item moja tu.

Kuna watu milion 100 ni kama elfu kumi tu. Na ndio maana anaweza kutoa Billion za kudhamini ligi na asiwaze.

Milion Mia per day kuna wazawa kibao wanakunja kirahisi tena kwwnyw item moja tu.
 
Kuna muda nilikuwa Zanzibar na mzigo wa nguo wa milion 50 natafuta mteja wa kumuuzia wote kwa jumla. Nilikaa nao Zanzibar ule mzigo zaidi ya wiki tatu... then nikaamua ngoja niupeleke kariakoo.


Huwezi amini nilikutana na jamaa akaona sample akaupenda hata hakwenda Bank jamaa alizama Shop akatoka na milion 50 kwemye begi. Aisee nilishangaa Sanaa kuna watu wana pesa pale Kariakoo nyie.

Na net profit ya 100 kwa siku kuna watu wanaikunja vizuri tu, tena watu wa kawaida akina Mo na Bakheresa hao ndio balaa.
 
hujakaa na kujua biashara kkoo ndio maana unabisha, ingawa biashara sasa hv imepoa sana hamna wateja kama zaman ila ilikua kuna watu wanaleta kontena hata 10 unakuta anatuma sample kwa wateja wiki kabla mzigo haujaingia sokoni yaani ukiwa bado bandarin na unakuta kontena 5 zimeshauzwa kabla hata hazijaingia sokoni na wateja wameshalipia benk mzigo ukishuka tu watu ni kubeba order zao walizolipia na risiti zao,
n.b ila sio kwa sasa baada ya soko kuharibika
 
mapato ya jumla 100M kwa saa wapo wwngi sana wanaingiza ila faida ya 100M kwa saa ni watu wachache wanapata sana sana wawekezaji wakubwa ndo wanaweza hiyo unakuta muwekezaji ndan ya saa anafanya biashara ya kuuza bidhaa za jumla kwa zaidi ya mikoa 15+ kwanini asipate hiyo faida
 
Kaluakoo nikawaida xana maana unakuta mtu anasambaza mizigo mikubwa mikoani na unakuta anawateja 50 mteja wakwanza huko alipo nimuuzaji wa jumla ambae anaweza mchangia mzigo wa milioni 50 mpaka 100 kwa siku mzigo ukitua nje ya hapo. Mtu anafremu mikoani anapangisha ana magari ya kukodisha kwahiyo kuna watu wanaingiza hiyo pesa kwa siku wapo wanaingiza kwa miki kwa mwezi ndo usiseme biashara zina siri
 
kiongozi million 100 ndogo sana kwa wafanya biashara watu wanaingiza milioni 500 kwa siku ijekuwa iyo 100.
Mil 500 kwa siku? Nani huyo?
Mil 500 kwa siku, kwa mwezi ni bil 15, kwa mwaka ni bil 180
Ingekua kweli basi Tanzania tungekuwa na mabilionea wengi sana. Mo mwenyewe kwa mwaka hafikishi hiyo pesa
 
Nimesoma comments na nimejifunza kitu kwamba:-
1. Watu hawaamini kwamba kuna biashara zenye pesa kulingana na circle yao ya kimaskini ilio wazunguka.

2. Hawaamini kubet ni biashara. Waakangakie takwimu za Ile kamari ya kurusha kindege kwa dakika ima make shingapi.

3. Matajiri ngozi nyeusi hujificha mno kiasi kwamba huwezi amini mfano Sawaya,Msigwa wa Super Feo.

4. Tembeleeni makaa ya mawe Njombe na Songea huko muone kua Kuna watu wanapesa mpaka hawajui wazifanyie nini.

5. Tunakosa exposure biashara ni mtaji.



Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Hayo yote hakuna asiyejua. Kinachobishaniwa ni kiwango
 
Kindege ile ni uongo yaani amna wa kuweka laki pale sijui laki mbili utapigwa mno...
 
Nauza Tshirt nzuri wakuuu za dukani reja reja 14k mzigo mzuri thsert nzuri nauza mapazia pia na vifaa vya ndani kwa bei nafuuu kwa uaminifu usisite kunitafuta
 
Nimefurahi sana nchi hii bado Kuna vijana wenye akili sana.

Hizi story za vijiweni za faida kwa siku sijui wanaokota wapi... fikiria hapo bado mali hujakopesha, hujaibiwa, hujalipa monthly expenses na bado gharama nyingine ambazo hukutarajia, mtu analeta Habari za faida ya siku... jamani😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…