Hivi kweli kuna cha kujifunza kutokana na uchaguzi wa Afrika Kusini kama taifa?

Sawa,Tuombe uzima.
 
Yes hivi vitu adimu ndio muhimu sana mkuu...


unadhani hali itawasaidia wa Africa kusini kusonga mbele?

naona ANC na EFF zikiunda serikali, lengo baadae ni kuunda chama kimoja chenye nguvu zaidi baadae kwasababu ni kabila moja....

naona uhasama wa ANC na MK Party ya ZUMA ni mbaya sana, lakini pia ANC na DA ni mahasimu wa kitambo sana pia sioni kama wanaweza kuunda serikali ya pamoja,

au mie naona kimakosa πŸ’
 
Si kweli, 23%( chama chenye mizizi wa wabaguzi) ndio walio wengi? Angalau wangefikia 40%, ningekuelewa.
Ukiangalia mijadala ya wasouth wameanza kuiona DA Kama suluhisho la matatizo yao. Halafu kumbuka kinavhofanya DA isipate asilimia hamsini ni ile chuki ya ubaguzi hapo tu.
 
Si kweli, 23%( chama chenye mizizi wa wabaguzi) ndio walio wengi? Angalau wangefikia 40%, ningekuelewa.
Wewe hushangai chama Cha kibaguzi kuwa Cha pili kwenye nchi ya waeusi asilimia 80 na zaidi?. Tafakali Hilo kwanza.
 
Ukiangalia mijadala ya wasouth wameanza kuiona DA Kama suluhisho la matatizo yao. Halafu kumbuka kinavhofanya DA isipate asilima hamsini ni ile chuki ya ubaguzi hapo tu.
thus why kongole nyingi sana zimuuendee Hayati Baba wa Taifa, Mwl.JK Nyerere aliimpact tunu njema na ya kipekee sana kwenye fikra na mioyo ya waTanzania mpaka leo hii mtoto wa dar anaweza kua na baba wa kichaga lakini, mtoto hajui kichaga kabisa na wala hana haja kujua. Anujua yeye ni Mtz inatosha....

ukabila unakwenda kufutika kabisa Tanzania baada ya miaka kadhaa ijayo πŸ’
 
Kwenye Press iliyopita ya EFF, Kiongozi wa EFF Julius Malema kadai wapo tayari kushirikiana na ANC. Shida ya huu Muungano wa ANC na EFF ni kwamba wote ni rejects. ANC kashuka mpaka asilimia 40, na huku EFF kashuka mpaka asilimia 9. Hivyo wakiungan itakuwa Muungano wa mabwege. Labda ANC aungane na MK hapo kidogo nguvu itarudi.

Pia Kwa taarifa za Chini Chini zinadai ya kwamba ANC na DA wapo kwenye maongezi ya awali ya kuunda serikali ya mseto ingawa itakuwa ngumu kidogo kwa wa ANC wenye msimamo mkali.
 
Tanzania ukabila hakuna sema Kuna watu wanalazimisha uwepo ila hakuna kabisa. Mimi kwa mfano sijui kuongea kilugha kabisa. Nadhani ukabila kutokuwepo Tanzania umetusaidia Sana Tanzania. Bila hivyo tungeishi kwa shida Sana.
 
Ni kama Nigeri wanavyohangaika kwa Sasa. Imebakia urais ni Kwa watu wa kaskazini maana ndio wengi. Wale wa kusini walipotaka kujitenga na kuanzanisha nchi ya Biafra Chini ya Dudumeju Ojwuku walishugulikiwa na jeshi la Nigeria. Mpaka Leo Nigeria haija settle wanawaona wa Igbo kama sio wanaigeria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…