Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Pamoja na ubovu wa katiba lakini lazima kuwe na seriousness katika maendeleo ya nchi. Tunaweza kuwa na viongozi wasiokubalika kidemokrasia lakini tupate maendeleo!
Maendeleo yanaanza kichwani kwako halafu Ndio yanasambaa duniani. Badilika kwanza wewe.
 
RPC ni kamanda wa Polisi wa Mkoa
OCD ni kamanda wa Polisi wa Wilaya
OCS ni mkuu wa kituo cha polisi
RCO ni Mkuu wa upelelezi polisi mkoa
OC-CID ni mkuu wa upelelezi polisi wilaya
Kama anko wako alikua OCD alikua Kamanda wa polisi wilaya.
RPC ni wilaya.

OCD ni wakuu wa vituo vya polisi. Mimi mwenyewe nina Anko amewahi kuwa OCD.
 
Ceremonial figures hizo

Chenga tu ,acha wachaguliwe position sio ya kimkakati (technical au managerial) unategemea nini
 
Kwa namna ulivyoteua ma-DC sioni kama uko serious. Nafasi ya u-DC inashuka hadhi kila kukicha, kwa sababu inaonyesha kila mtu anaweza kitu ambacho si kweli.

DC ni mtu ambaye anatakiwa atoe dira ya maendeleo ya wilaya yake lakini kwa baadhi ya hawa uliowateua ni sawa na wapiga debe wa daladala! DC ni mtu ambaye anatakiwa kumshauri RC kudumisha amani ndani ya wilaya yake lakini hawa ni ma-DJ watakaokesha katika kumbi za starehe. DC ni mlezi wa vijana katika wilaya yake lakini hawa ni comedians.

Kwa kifupi hakuna uongozi katika wilaya, hakuna mlezi, hakuna busara uliyopeleka wilayani bali kuna washereheshaji! Tafadhali Rais Samia hebu kuwa serious kidogo wananchi tupate imani! Nalilia nchi yangu inavyoangamia! Hawa vijana wako angalau wangepewa orientation ya uongozi!

Mungu ibariki Tanzania!
Vijana wa Arusha waliona DC anakuwaje ,Kenan Kaacha Legacy wasioishi Arusha Mjini hawawezi elewa nanchosema .
 
Ni afadhali mara milioni moja kuwa na wapaka poda katika hiyo nafasi kuliko watu aina ya Sabaya, bashite, Odunga, Byakanwa n.k
Nilipata shida kidogo kuiweka nilivyoiweka; kwa sababu mwanzo nilitaka kuiweka kama ulivyoiweka hapa wewe.

Kwa vyovyote na iwavyo, hakuna nafuu kokote.
 
DC haleti maendeleo ya nchi, kazi yake ni kuleta maendeleo ya chama
 
DC ni cheo ambacho hata kisipokuwepo hakuna kitakachokwama.

Sema maRPC ndio watakaopata tabu, imagine utatakiwa kuwaheshimu hao kama wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama🤣

Uaskari ni kazi ngumu sana.
A u serious?
 
Women should never lead men in power, politics and authority. Hayo ndiyo matokeo yake ......
Achana na hizi concepts za kilofa. Wanaoidhinisha nchi za Africa zipewe misaada baadhi ni mawaziri wanawake.

Bosi wa sasa wa EU ni mama, ukiona nchi yako imepewa msaada na jumuiya hiyo siku za karibuni tambua aliyeidhinisha ni mwanamke.
 
EeeenHeeee!

Nacheka huku nikilia machozi kwa nchi yangu Tanzania.

Tunatoka kwenye kikaango tunaangukia kwenye makaa ya moto mkali.

Mungu Ibariki Tanzania.
Tuliza mshono upate akili, maana tulipokuwa tunakuambia ya maana ulituona wapuuzi.
 
Yaani kwako wapiga debe hawafahi unataka maprof siyo? Acha tuendelee na wapiga debe wa daladala ndiyo wanajua tatizo la wananchi.
Kwa kifupi nataka tuwe na viongozi makini!
 
Sijaona majukumu ya kutisha ya DC hata mwanangu anaweza kupewa hicho cheo. Nachoona ni upotevu wa rasilimali za nchi bora kingefutwa hizo hela zikajenge barabara huko vijijini.
 
MKOA WA DAR UNAHITAJI maDC WAZOEFU. SASA UNAMCHAGUA HERI JAMES NA FATMA ALMAS WAJE WAJIFUNZIE DAR? SI WANGEANZIA NAMTUMBO AU URAMBO HUKO
Hiyo nafasi haihitaji uzoefu hata wewe tukikupa ukuu wa Mkoa sasa hivi unafanya bila tabu yeyote.ninachokiona ni hizo nafasi zifutwe maana hazina kazi.
 
Yaani kweli Nikki wa Pili anaenda kulisimamia na kuwa juu ya jeshi la polisi la wilaya pamoja na maafisa usalama wilaya???
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Kwani anawabeba mgongoni? Kwanza niki ni kijana msomi kuliko hata ma DC wengi walioteuliwa.ingawa usomi na uongozi vitu viwili tofauti.
 
Hiyo nafasi haihitaji uzoefu hata wewe tukikupa ukuu wa Mkoa sasa hivi unafanya bila tabu yeyote.ninachokiona ni hizo nafasi zifutwe maana hazina kazi.
Vinginevyo wanatakiwa wapigiwe kura na wananchi
 
Back
Top Bottom