Mnavyojadili utafikiri mna uwezo wa kujiongeza hata unywele mmoja tu. hao mnaowasema na sauti gani sijui hawakujiumba. hivyo hivyo na kwa wanawake wenye sauti za kiume, wanaume wasio na ndevu vs wanawake wenye ndevu, au sisi wanaume weney garden love vs wengine ambazo pengine hawana garden, warefu kwa wafupi, wanene kwa wembamba, weusi na weupe n.k. hayo yote ni Mungu amefanya, cha muhimu tu wewe kama ulizaliwa mwanaume uishi kama mwanaume, and vise versa is true.
Kenya kuna dada mmoja anaitwa Sara Kiarike (wengi humwita Sara K), anaimba vizuri sana. inasemakana alizaliwa pacha na mwenzake, mwezie alikua na uwezo sana darasani, yeye hakuwa na uwezo, mwenzie alipendwa yeye mara nyingi alikuwa akishindwa anatukanwa " lisauti lako kubwa", Mungu alimpandisha polepole kwa lile lile lisauti likubwa kama la mwanaume likiimba akawa mwanamziki mkubwa sana anayeimba hata kwenye hafla za kitaifa mbele ya Rais wa nchi. Anajulikana na kuheshimika duniani kuliko hata mwenzake ambaye hata hatumjui.
hapo ndipo nilijifunza kutobagua watoto wala kuonyesha kumpenda huyu zaidi ya mwingine. mwanangu hata akifelis huleni kuliko wenzake huwa simkatishi tamaa, namwambia mbona umejitahidi tu, siku nyingine utafanya vizuri zaidi ya hivi, kazana. basi, ila siwezi kumwambia wewe huna akili kuliko fulani au kwanini fulani amefauli wewe umefeli?