Hivi Lazaro aliyefufuliwa na Yesu, alitoa ushuhuda gani kuhusu kuzimu baada ya kufufuka?

Kuzimu ni kaburini.
Aliibuka kama mtu aliyetoka kulala.
Angekuwa mahali bora angeibuka na kumalumu Yesu kwa nini kamrudisha kwenye shida za dunia?
Uzuri zaidi Yesu alisema Lazaro alilala usingizi katika kifo na alimfufua au alimuamsha kutoka usingizi wa kifo. Nothing going on alipokufa na alipofufuliwa hakueleza lolote... Muhimu Yesu alisema aliamka usingizi katika kifo
 
😆😆😆😆😆
 
Lazaro wapo wawili
 
Mkuu kwa hii Kasi yako ya kuichunguza biblia, sioni kama utaendelea kuhudhuria kanisani. Mimi baada ya kuanza kujiuliza maswali kama yako, kwa sasa nimebaki mromani mstaafu. Naongea na Mungu direct sitaki tena hivyo vitabu.
Tumepewa akili na marifa ila kuhoji mambo haya ni kukufuru Mungu.

Leo hii nimesikio clip ya Mchungaji mmoja maarufu sana(Mchungaji Daniel Mgogo) ambae clip zake husambaa sana mitandaoni akisema, "waliodai Israeli ni Taifa teule,ni Manabii wa Kiyahudi".

Sasa hyu Mchungaji nae anahoji/anapingana na maandiko kama kina sisi?

Mambo mengi muda mchache.
 
Ulimuhoji Lazaro!?
 

Kabla ya kuchangia chochote kwenye uzi huu, nina maswali haya kwanza...

1. Je, unamwamini Yesu Kristo?

2. Je, unaamini katika Biblia?
 
Kabla ya kuchangia chochote kwenye uzi huu, nina maswali haya kwanza...

1. Je, unamwamini Yesu Kristo?

2. Je, unaamini katika Biblia?
Maandiko yananichanganya sana na kwakweli niko katikati kama yote tunayoyasoma katika vitabu hivi ni ya kweli.

Cha jabu zaidi, leo hii viongozi wa dini huko Ulaya(kanisa la Anglican) kwa mujiubu wa BBC, nao tunaambiwa wameanza kutambua ndoa za jinsia moja wakati maandiko yanakataza na tukumbuke hizi dini zimeletwa na hawa hawa wazungu.

Sasa mpaka hapa huoni kuna mashaka makubwa?

Je, inawezekana vioingozi hawa wa dini wa huko Ulaya wanajua siri ambazo sisi waumini weusi hatuzijui na mojawapo inawezekana kuwa maandiko kuhusu ushoga hayakutoka kwa Mungu ndio maana leo hii wanaenda kinyume na maandiko hayo japo ushoga unatia kinyaaa?
 
Muda mwingine ukilala hata kama umeota vipi ilq hasubuhi ukumbuki chochote kile,pia yupo jamaa mmoja aliwahi sema,kifo hatukutani nacho ila walio hai ndo wanamuona mtu kafa na ndo wanaoumia na kujiuliza maswali mengi ya kijinga kama yako hayo!!!
 
Yule aliyekula makombo je? Biblia inasema alikufa wakakutana na tajiri mbinguni
Ule ni mfano tu. Si jambo halisi. Kuna somo refu pale, unatakiwa kuanza kusoma mistari kadhaa nyuma kujua Mwana wa Mungu alikuwa anazungumzia nini.
 
Yule jamaa ni stad up comedian. Hana uchungaji wowote.
 
Unajuaje alikuwa kuzimu?
 
Hayo maelezo ni ya Yesu mwenyewe na kumbuka Yesu alifundisha kwa mifano.
 
Kifo ni kama Usingizi mzito. Ndiyo maana Yesu aliwaambia rafiki yetu Lazaro amelala ila naenda kumuamsha. Wakamwambia, "Kama kalala si ataamka!" Lakini Yesu alikuwa anamaanisha kafa. Ukifa huna tofauti na mtu aliyelala fofofo.
Kulala; more appropriately kulala mauti ni njia nyingine (polite way) ya kusema kafa. Haimaanishi kufa ni sawa na kulala fofo ambako hata kuoza mtu haozi tofauti na kufa.
 
Soma kitabu kinaitwa Injili ya
Nicodemus Kila kitu kimeandikwa humo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…