Vizuri mkuu,wacha nipite kwenye point zako.
Kipengele cha kwanza na chapili na kubali,japo China naye ameshaanza kupiga hatua kuja juu katika hizo sehemu,na hatua yake ndio inayomuumiza kichwa USA.
Tukija katika masuala ya kitiba kiujumla iwe biotech,pharmaceuticals iwe masuala ya epidemiology China kapiga hatua kuliko USA.
Kama ulifuatilia Corona China ilichukua siku 90 kuidhibiti corona,vifo vilipungua na maambukizi yalikua yenye kudhibitiwa.
Vifo vingi vilitokea mwanzo wa eruption ya Covid 19.Ila baadae China iliweza kudhibiti usambaaji wa Corona.
Tukija kwa USA,Spain na Italy ndio waliokuja kuongoza kwa vifo na iliwachukua muda kudhibiti Corona.
China ndio nchi pekee ulimwenguni wenye uwezo wa kupambana na aina nyingi za saratani tena kwa tiba za kisasa na kienyeji.
Na ulimwenguni China pekee ndiye aliyeendelea katika herbal science.
Upande wa afya China yuko mbele zaidi kaifuatilie mkuu.
Kuhusu aerospace nakubali japo China anapiga hatua kali kuja hilo eneo katika fighter jets kashakamilika ila katika ndege za abiria bado ndio anajitafuta ila soon anakuja walipo wengine.
Kuhusu dollar kuwa medium of exchange hilo halipingwi kuna factors nyingi zinazofanya dollar bado kuwa na nguvu,japo kukosekana kwa dollar kunatuathiri sisi nchi za ulimwengu wa tatu.
Kuhusu manufacturing CHINA HANA MPINZANI,China is the most industrialized nation na inachangia zaidi ya 32% ya manufacturing goods ulimwenguni,kalifuatilie hili mkuu.
Kiubora China huwenda anazidiwa na Germany na Japan ila sio USA.
China ana uwezo wa kuunda bidhaa zenye ubora kama wa USA na amethibitisha hilo katika soko.
Tesla EV zimeonekana kuwa na ufanisi mdogo chini ya Chinese EVs.