fidel castro wapili
JF-Expert Member
- Mar 18, 2017
- 3,497
- 2,911
Litakuwa ndio anguko lahuyo taperi USAMarekani na washirika wake wa ulaya lazima waporomoke na upepo utahamia china, Russia pamoja na waarabu yaani BRICS.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Litakuwa ndio anguko lahuyo taperi USAMarekani na washirika wake wa ulaya lazima waporomoke na upepo utahamia china, Russia pamoja na waarabu yaani BRICS.
Kweli, Lakni kumbuka aliyopo nyuma ya USA ndyo huyo huyo yupo nyuma ya BRICS. Unajuwa ni nani huyo?Litakuwa ndio anguko lahuyo taperi USA
Kwa hiyo taifa la china ni ile race au registered citizens? Sasa hizo we chat kwa nini zisiwe maaarufu duniani Kama x na nyinginezo?Harmony operating system unaijua wewe ?Hao wana vita ya kibiashara hata wanasayansi wa Marekani ni kutoka mataifa ya nje😛😛
Kuna wechat na mitandao kibao , waulize wanaofanya biashara kwenda china wanatumia mitandao gani sio takataka zako zinazohackiwa mpaka watu wanasambaza porno huko fecebook .
Mrekani anawatumia china na mataifa mengine kweny kupata teknolojia hata mashindano , wewe kajamba nane kutoka kyela unapiga kelele
Tiktok ni maarufu kuliko hizo takataka nyingine, wechat inatumika china mtandao wao ahwaatumii vya mzungu , nenda korea wana mitandao yao .Kwa hiyo taifa la china ni ile race au registered citizens? Sasa hizo we chat kwa nini zisiwe maaarufu duniani Kama x na nyinginezo?
Mchina kazi yake ni ku-copy ama kuiba kwa hao hao wama gharibi.Labda Mimi elimu yangu ndogo, Mchina ana technology gani ya kumzidi USA🇺🇸
Nikiangalia wale mabwana kila sector wapo vizuri.
1) Upande wa ndege hawana mpinzani
2) Mambo ya space science ni hatari
3) Magari ni hatari
4) Micro chips usiseme
5) Computing hawana mpinzani
6) Kwa kilimo ni hatari
7) Kwenye madawa wamo
8) Ujenzi ni hatari
9) Technology ya simu wanatisha
Na mengine mengi tu. Sasa Mimi najiuliza Mchina ana kitu gani cha kuwazidi hawa mabwana.
Upande wa Uchumi kuna gap kubwa mno. USA ana 28.7 trillion USD GDP. Mchina ana 18.5 trillion USD GDP. Gap hiyo ni kubwa.
Anguko LA USA sio Leo wala kesho. Labda miaka Mia mbili Ijayo
Mkuu unadhani mtu wa Low income wa leo ataendelea kuwa wa Low income miaka ijayo , ukimuona mtu kanunua kitu cha bei rahisi sio kwasababu anakipenda ila ni kwamba hela hana , siku akiwa nazo jua huyo sio mteja wako.Marekani bidhaa zake anajikita hasa soko la high class hivyo production yake haijikiti sana kwenye mass production Kwa ajili ya Dunia nzima class za chini .Mchina kajikita kwenye mass production Kwa ajili ya low class ambao wako wengi Dunia nzima ndio majority ya Dunia kuhakikisha wanapa bidhaa affordable
Na anapata faida kweli kweli Kwa mass sales
Lengo la china ni ku dominate soko la low income people kuhakikisha hakuna wa kupenya
Upo kishabiki sana mkuu impact ya hio Belt Road and initiatives ni ipi haswa , USA inalazimika kuziwekea baadhi ya kampuni za China kutokana na Sera za taifa ,China kampuni inaweza kuwa na nguvu lakini bado mambo yake mengi yanakuwa influenced na Serikali ,unadhani communist party ikiamua kutaka kupata taarifa za mtumiaji flani wa Tiktok wa Kimarekani inashindwa ,ogopa sana kampuni ambazo zipo chini ya sera ya Socialist Market economy.Hakuna sanctions ambazo USA alimuwekea China zikafanikiwa.
Bali hum back fire tu.
Rejelea kuanzai 5G na Huawei na ishu ya ushuru bandarini.
USA aliathirika kwa kiasi kikubwa pale China alipokataza raw materials zake kutokwenda viwanda vya USA.
Tiktok kuifungia uache kazi ufanye kazi,maana USA ataitaji sapoti ya ULAYA na Ulaya sasa hivi wanamiminika China kuunda nae muungano wa kidiplomasia na kibiashara.
Fuatilia kitu kiitwacho BELT AND ROAD INITIATIVE.
Yani kwasasa USA ni joka la kibisa.
China hatoweza kumzidi USA in which aspects!?Upo kishabiki sana mkuu impact ya hio Belt Road and initiatives ni ipi haswa , USA inalazimika kuziwekea baadhi ya kampuni za China kutokana na Sera za taifa ,China kampuni inaweza kuwa na nguvu lakini bado mambo yake mengi yanakuwa influenced na Serikali ,unadhani communist party ikiamua kutaka kupata taarifa za mtumiaji flani wa Tiktok wa Kimarekani inashindwa ,ogopa sana kampuni ambazo zipo chini ya sera ya Socialist Market economy.
Dunia inakoelekea haihitaji Socialist Market economy bali inahitaji free market economy na Marekani licha ya kuwa kwenye Mixed Economy ila uhuru wa kisoko upo.
Hebu nenda kafuatilie Hotuba ya Raisi wa Argentina Javier Miller juu ya Free Market economy kwanza.
China haitoweza kumzidi Marekani labda itokee aondokane na mfumo wa kikomunisti na kuingia kwenye Pure Capitalism.
Wanatumia zile zile za, magharibi, lakini wanazalisha bidhaa kwa bei nafuu, mfano kwenye EVs electrical vehicles, Za, china zina bei nafuu kuliko za, America na ulayaLabda Mimi elimu yangu ndogo, Mchina ana technology gani ya kumzidi USA🇺🇸
Nikiangalia wale mabwana kila sector wapo vizuri.
1) Upande wa ndege hawana mpinzani
2) Mambo ya space science ni hatari
3) Magari ni hatari
4) Micro chips usiseme
5) Computing hawana mpinzani
6) Kwa kilimo ni hatari
7) Kwenye madawa wamo
8) Ujenzi ni hatari
9) Technology ya simu wanatisha
Na mengine mengi tu. Sasa Mimi najiuliza Mchina ana kitu gani cha kuwazidi hawa mabwana.
Upande wa Uchumi kuna gap kubwa mno. USA ana 28.7 trillion USD GDP. Mchina ana 18.5 trillion USD GDP. Gap hiyo ni kubwa.
Anguko LA USA sio Leo wala kesho. Labda miaka Mia mbili Ijayo
Una mahaba ya ajabu ngoja nikwambie tech nyingi zilizopo leo chanzo ni USA hilo huwezi kataaTiktok ni maarufu kuliko hizo takataka nyingine, wechat inatumika china mtandao wao ahwaatumii vya mzungu , nenda korea wana mitandao yao .
Nimekuambia uliza watu wanaoagiza vitu china mara nyingi wanatumia mtandao gani, ile Alibaba ni mzungu sio?
Maeneo ambayo Mchina kaachwa mbali :China hatoweza kumzidi USA in which aspects!?
Kama ni trade amekwishamzidi mkuu,siongei kishabiki naongea nachokijua buddah.
Tuanzie ushawishi wa kibiashara/kifedha,Benki kuu ya China inaonekana kuwa ni bora na nafuu kulipa kuliko IMF/WB.
Mpaka sasa China imekopesha mataifa 138+ na kusamehe mataifa 38 madeni,na bado mataifa yanamiminika kukopa China na ukanda unaomiminika ni wa South East Asia,Eastern Europe na South America.
Kibiashara China hakuna sehemu bidhaa zake haziukizi,tena hususan Afrika ndio tumejaza bidhaa za Mchina kuliko bara lolote.
-Kidiplomasia China amekua mwenye kusikilizwa sana kipindi hiki,na hata baadhi ya migogoro yeye ndio amekua mtatuzi,mataifa mengi sasa hivi masuala ya kidiplomasia hufanya reference ya China,na wanaipongeza China kwasababu haingilii ITERNAL SOVEREIGNTY ya taifa lolote,sio kama USA anaenda mbali kiasi kufadhili mapinduzi ya serikali za watu.
Ni wapi unasema China hajamzidi USA?
Belt and road initiative ni mpango wa kibiashara na ujengaji wa miundombinu kwa gharama nafuu baina ya China na mshirika wake yeyote atakayehitaji kuingia nae makubaliano.
Eastern Europe imejengwa sana na China kupitia Belt and road pia biashara nyingi Eastern Europe zime prosper kwa initiative ya belt and road.
Namalizia kusema hivi mkuu,China sio taifa jepesi kama udhaniavyo.
Kaa lifuatilie vizuri mkuu.
Chancellor wa Germany kwenda China hakuwenda kiwepesi.
France officials kwenda China hawakuenda kiwepesi,tena inasemekana ni zaidi ya 20+ years hao watu hawakukanyaga China.
We endelea kuwa understimate mkuu.
Vizuri mkuu,wacha nipite kwenye point zako.Maeneo ambayo Mchina kaachwa mbali :
1.Semiconductor.
2.Software development
3.Biotechnology and Pharmaceutical: Mfano tu maswala ya Corona.
4.Aerospace : Hapa China anakuja kuja nyuma ya Mrusi, baba yake USA yuko mbele .
Hivyo ni vipengele vichache tu upande wa Tech , twende kwenye international trade hapa Dollar ya Kimarekani katika ku'conclude international transfer hana mpinzani , China amefanya counterattack kwa kutengeneza BRICS na mwenzake Mrusi lakini Dola haijadeppreciate value yake , Uliza wafanya biashara wa Bongo walivyokuwa wakihaha kuitafuta Dola Benki ili wakafungashe.
Makampuni makubwa ya International transaction yapo chini ya Wamarekani hapa tunapoongea una Kadi yako ya Mastercard Au Visa Card mfukoni , Hio kadi ipo chini ya Mmarekani.
Upande wa Product manufuctering China anamfukuzia kwa nyuma Mmarekani sikatai lakini ukweli ni kwamba yupo nyuma sana kwenye swala la Ubora wa Bidhaa zake.
Kijeshi hapa haina haja ya Kuongea ukienda Japani unaikuta Kambi ya Jeshi la Marekani , Ukienda Korea unaikuta bado hujazungumzia teknolojia ya Siraha na kuendelea, Bado hujazungumzia NATO na mengineyo.
Ni kweli China imepiga hatua kwenye mambo mengi lakini tusiongee kishabiki kiasi cha kuexaggarate facts
Kuhusu jeshi kaka wacha nimalizie.Maeneo ambayo Mchina kaachwa mbali :
1.Semiconductor.
2.Software development
3.Biotechnology and Pharmaceutical: Mfano tu maswala ya Corona.
4.Aerospace : Hapa China anakuja kuja nyuma ya Mrusi, baba yake USA yuko mbele .
Hivyo ni vipengele vichache tu upande wa Tech , twende kwenye international trade hapa Dollar ya Kimarekani katika ku'conclude international transfer hana mpinzani , China amefanya counterattack kwa kutengeneza BRICS na mwenzake Mrusi lakini Dola haijadeppreciate value yake , Uliza wafanya biashara wa Bongo walivyokuwa wakihaha kuitafuta Dola Benki ili wakafungashe.
Makampuni makubwa ya International transaction yapo chini ya Wamarekani hapa tunapoongea una Kadi yako ya Mastercard Au Visa Card mfukoni , Hio kadi ipo chini ya Mmarekani.
Upande wa Product manufuctering China anamfukuzia kwa nyuma Mmarekani sikatai lakini ukweli ni kwamba yupo nyuma sana kwenye swala la Ubora wa Bidhaa zake.
Kijeshi hapa haina haja ya Kuongea ukienda Japani unaikuta Kambi ya Jeshi la Marekani , Ukienda Korea unaikuta bado hujazungumzia teknolojia ya Siraha na kuendelea, Bado hujazungumzia NATO na mengineyo.
Ni kweli China imepiga hatua kwenye mambo mengi lakini tusiongee kishabiki kiasi cha kuexaggarate facts
Anasuasua au wanamuundia zengwe asuesue!?Mkuu unadhani mtu wa Low income wa leo ataendelea kuwa wa Low income miaka ijayo , ukimuona mtu kanunua kitu cha bei rahisi sio kwasababu anakipenda ila ni kwamba hela hana , siku akiwa nazo jua huyo sio mteja wako.
Hio Mass production unayozungumzia ni kwa hapa Africa tu , ndio soko ambalo mchina anatengeneza kila uchafu na kuwatelea vingine vina hadi madhara ila ndio hivyo huwezi ona madhara yake kwa muda mfupi..
Bidhaa zote ambazo mchina anapeleka Ulaya , Amerika ya Kusini na Kaskazini ni high quality na huko anasua sua maana watu washamonopolise soko
Approach ya Vita miaka 50 na sasa hivi ni tofauti sana , ,teknolojia imepiga hatua , Vita za Enzi hizo zimekuwa historia katika vitabu na sio kwenye uwanja wa VitaKuhusu jeshi kaka wacha nimalizie.
China ni jeshi lenye silaha bora na zenye ufanisi pia,isipokua haiji promote kama USA.
Hivi unajua kama USA na China waliwahi pimana ubavu kupitia proxies na USA akashindwa!?
Rejelea vita ya Korea war 1950s.
Jeshi la China iliisaidia North Korea na 1959 USA ilipoteza askari wengi sana Jangsari kiasi ili retreat mpaka eneo ambalo sasa linaitwa demilitarized region.
Ndio maana Kule South China sea China kapora mipaka ya maji ya Phillipines ila USA hakufanya hatua yeyote.
Silaha za China zimeuzwa na kufanya ufanisi sehemu nyingi sana.
Technology ya silaha anayotumia North Korea 90% ni kutoka China.
Kamfuatilie huyu jamaa anaitwa NAPOLEON BONAPARTE,aliwahi kusema "China is a sleeping lion,if when it wakes the world will shake".
Sawa mkuu ila mbona China anauza silaha nchi tofauti na zinafanya kazi?Approach ya Vita miaka 50 na sasa hivi ni tofauti sana , ,teknolojia imepiga hatua , Vita za Enzi hizo zimekuwa historia katika vitabu na sio kwenye uwanja wa Vita
Sasa hivi China kuwa na teknolonia kubwa kwenye Siraha imekuwa ni kama Uvumi tu kwasababu hatujaziona zikiwa zinafanya kazi, Ni kheri Mmarekani ambaye anajaribisha baadhi ya Siraha zake pale Ukraine kwa kigezo cha kutoa msaada.
Kuilinganisha nchi na nchi kijeshi ni swala Complex sana kwasababu hakuna nchi ambayo itaweka wazi teknolojia zake
Ukishaelewa Biashara ni Vita mkuu umefanikiwaAnasuasua au wanamuundia zengwe asuesue!?
Kivipi embu nieleweshe?Ukishaelewa Biashara ni Vita mkuu umefanikiwa
Mngekuwa mnafuatilia na kujua mambo mengi ya nchi zenu tungekuwa mbali. M'bongo ukitaka aharishe kila kitu na aingie kwenye mjadala mletee mijadala ya aina hii. 1. Kati ya fulani na fulani nani ni tajiri zaidi? Kati ya nchi fulani na fulani ipi imeendelea zaidi?Sio kwamba ana teknolojia gani kumzidi USA, bali speed yake ya kucatch up ndio inamtishia USA. Yani kwa muda mfupi alikotoka na alipo sasa ndio hatari hiyo hili linaonyesha kuwa anaweza kumfikia na akampita.
Wakati Huawei wameilima sanctions, wao wamarekani walihisi walau aaweze kubreak through itakuwa 2028, ila wakaja kushangaa hata miaka 3 haijaisha Huawei katengeneza chip zake. Yani ilikuwa ni kama kitu impossible. Jana nimeona habari kuwa wamebreak through kwenye chip ya 5nm so simu itakayofuata itakuwa na 5nm na kumbuka kuwa wengine US wako 3nm ila shida sio hawa kuwa 3nm shida ni kwamba na vikwazo vyote hivyo bado jamaa wana catch up kwa haraka.
Samsung na LG walikuwa wamekamata soko la screen panels, TCL sasa hivi anatisha huko. EVs mchina now kashachukua taji, Meli ndiye anayeunda nusu ya order zote za meli duniani. Research papers kapublish za kutosha, Drones anauza drones nyingi.
Steve Jobs aliwahi kusema, wao wanazalisha iPhones china kwa sababu ukienda china ukataka watu wanaojua kitu fulani watajaa uwanja wa mpira ila USA inawezekana hata meza wasijae. Wachina wako aggressive na ule udikteta wa serikali unaweza kuwaongoza wana nchi kuelekea kokote wanakotaka bila kupinga.